Riwaya ya Chinua Achebe, Things Fall Apart, inafahamika duniani kote. Inatumika sana mashuleni. Mimi kama mwalimu wa fasihi nimefundisha riwaya hii kwa miaka mingi, hadi nikaandika mwongozo kwa wasomaji, wanafunzi, na walimu. Mwongozo huu ni kijitabu ambacho kinapatikana mtandaoni. Bofya hapa.
Lakini, kama watu wasemavyo, tunakwenda na wakati. Tarehe 1 Novemba, 2009 nimekichapisha kijitabu hiki kama "e-book." Yeyote mwenye kifaa kiitwacho "e-reader," au "e-book reader," anaweza kukiingiza katika kifaa hicho, akakisoma. Bofya hapa.
2 comments:
prof, nashinddwa kuchapisha vitabu bwana. kila nikijaribu sijaweza ila ntafanikiwa tu, sijajua kama ni lazima uwe kwenye PDF au la
Hebu ngoja nihangaike na shughuli zinazonikabili kwa sasa, halafu nitakuandikia maelekezo. Nikichelewa baada ya wiki moja hivi, nibonyeze.
Post a Comment