Wednesday, June 20, 2012

Nimetua Bondeni, kwa Madiba

Tarehe 14, nilitua Johannesburg, kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na American Council of Learned Societies (ACLS). Mkutano tumefanyia katika chuo Kikuu cha Witwatersrand, ukiwa umehudhuriwa na watafiti kutoka Afrika Kusini, Ghana, Marekani, Nigeria, na Tanzania. Tulijadili mada za utafiti zilizowasilishwa na watafiti mbali mbali. Utafiti huo hugharamiwa na ACLS, kwa wale ambao miradi yao ya utafiti inaonekana kuwa ya kiwango kinachotakiwa. Mada zote zilikuwa katika nyanja mbali mbali za sayansi ya jamii.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kila la kheri na mpe salamu babu Madiba!

Christian Sikapundwa said...

Tunakutakia mkutano wenye matokeo mazuri kama bado haujarudi Marekani au Tanzania.

Mbele said...

Asanteni. Nilisharudi Tanzania ile tarehe 18. Nina picha nilizopiga kule Johannesburg ambazo ninataka kuziweka hapa kwenye blogu, ila kamera yangu inakorofisha. Jamaa mmoja amenishauri niende Mlimani City hapa Dar nikawaone wataalam. Napangia kwenda leo.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...