TAMKO LA CCM MKOA WA MOROGORO KUHUSU VURUGU ZILIZOTOKEA RUAHA JANA JIONI
Ndugu
wananchi Tarehe 24/4/2013 ulifanyika uchaguzi wa mwenyekiti wa Serikali
ya kijiji cha Ruaha. Vyama vilivyoweka wagombea vilikuwa CCM na
CHADEMA. Hata hivyo mgombea wa Chadema alienguliwa baada ya CCM
kumuewekea pingamizi kwa sababu alikuwa na mapungufu yaliyomwondolea
sifa ya kuwa mgombea kwa mujibu wa sheria. Hivyo basi CCM ilitangazwa
mshindi na siku hiyo hiyo Chadema wakashinda kitongoji.
Wana
CCM waliyapokea matokea bila vurugu na wakakubali kuwa Mwenyekiti wa
Kitongoji ni wa CHADEMA. Tarehe 09.05.2013 ili kuwa siku ya kukabidhiwa
rasmi ofisi kwa Mwenyekiti mpya wa Kijiji cha Ruaha, lakini wenzetu
CHADEMA wakataa kumkubali huyo Mwenyekiti na wakaamua kuanzisha vurugu
kubwa sana katika kijiji cha Ruaha na maeneo ya karibu yaliosababisha
uharibifu mkubwa wa mali.Wamechoma nyumba, wamefunga barabara na
kusababisha uvunjifu mkubwa wa amnai eneo hilo.
Tunalaani
sana vurugu hizo zilizosababishwa na kundi la watu wenye nia mbaya na
nchi hii wanaotaka kuivunja amnai tulionayo, wananchi wa morogoro na
Watanzania kwa ujumla Tunavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua
hatua mara moja kurudisha amani ili wananchi waendelee na shuguli zao za
kila siku za kujiletea maendeleo. Kwa wale wote waliochochea vurugu
hizo wachukuliwe hatua mara moja na sheria ichukue mkondo wake.
Imetolewa CCM Morogoro
10.05.2012
No comments:
Post a Comment