Thursday, May 23, 2013

Mkutano wa Watu Wenye Asili ya Afrika, Minnesota

Leo nilienda St. Paul, kushiriki katika mahojiano kuhusu watu wenye asili ya Afrika wanaoishi Minnesota.

Watu kadhaa walihojiwa, kila mtu peke yake, na mahojiano yamerikodiwa ili hatimaye itangenezwe video ambayo itaonyeshwa kwenye mkutano utakaofanyika tarehe 28, 29, 30 Juni. Mkutano huo, ambao unaratibiwa na Minnesota Humanities Center na Council on Black Minnesotans, utakuwa na mijadala na maonesho kuhusu watu wenye asili ya Afrika, kama vile historia, siasa, utamaduni.

Aliyeandaa mahojiano ya leo ni Tene Wells, ambaye amefanya kazi kubwa. Katika picha inayoonekana hapa, tuko baadhi ya watu tulioshiriki shughuli ya leo. Kutoka kushoto ni Adebayo, Joseph Mbele, Tene Wells, Profesa Mahmoud el-Kati, na Adrian Mack.

No comments:

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...