Monday, July 31, 2017

Duka la Vitabu la Tanzania Publishing House

4 comments:

Emmanuel Kachele said...

Asante sana Profesa. Vitabu ni muhimu sana. Lakini huku vijijini hatuna na hata wale wenye nia ya kusoma hawapati vitabu. Ningeweza ningeishauri serikali ifungue maktaba kila shule na kila wilaya ama tarafa.

Mbele said...

Ndugu Emmanuel Kachele

Shukrani kwa kupita hapa kwenye blogu yangu na kuandika ujumbe. Nami, kwa miaka na miaka, nimekuwa na mtazamo kama wako kuhusu wajibu wa serikali kusambaza maktaba nchini. Angalia jiji la Dar es Salaam, kwa mfano. Jiji limekua sana na linaendelea kukua, lakini sijawahi kusikia serikali ikiongelea kufungua maktaba. Ilitakiwa kuwe na maktaba angalau katika wilaya zote tatu.

Jambo jingine ni kuwa serikali yenyewe haihamasishi usomaji wa vitabu. Katika matamasha ya vitabu, kwa mfano, viongozi wa serikali, mawaziri, wakuu wa wilaya, na wanasiasa kwa ujumla hawaonekani. Wanaoonekana ni zaidi wanafunzi na waalimu.

Hata vitabu vya Mwalimu Nyerere sidhani kama hao tunaowaita viongozi wamevisoma au wanavisoma. Sijui ni wangapi wanaweza kutaja majina ya vitabu angalau vitatu vya Mwalimu Nyerere. Ninaongelea kutaja majina tu ya hivi vitabu, achilia mbali kuvisoma. Hata hotuba zao hazionyeshi kuwa wanasoma vitabu, wakawa wanafahamu masuala mbali mbali ya siasa, historia, uchumi, falsafa, saikolojia, sayansi, tekinolojia, ukoloni mamboleo, utandawazi, na kadhalika.

Suala hili la umuhimu kwa viongozi kuhamasisha usomaji wa vitabu nimeliongelea katika blogu hii tena na tena. Mfano ni jinsi nilivyomwongelea Rais Obama.

mwanammuni said...

Salamu!
Natanguliza shukrani kwa mjadala muhimu uliotolewa.
Mimi ninaishi kijijini, mmnayoyaongelea ninayaona kila uchao. Lkn napenda kuwajulisha maajabu ya huku ni watanzania watumishi ndiyo wasiopenda kusoma vitabu wakidai wako busy! Wakati kimtazamo, hao ndiyo wasomi. Sasa tutafanya vipi uhamasishaji wa usomaji wakati wahamasishaji hawasomi?
Naomba msadiki ninayoyasema; pale vitabu vya kitaaluma vinapofika kwa wasomaji vikiwa na makosa ya wazi wazi lkn kuna sahihi za wataalam waliovipiti. Makampuni ya uchapishaji yanafanyakazi ya kuandaa lesson plan na "kuprint" vitabu vya wanafunzi badala ya vitabu vya wanajamii na maendeleo. Maktaba zilizopo hazina wasomaji! Labda wasomi wa siku nyingi mtujuze zile mbinu mlizozitumia zamani zilizopelekea kupata maktaba chache na zikatumiwa! Mi sielewi ujue, natamani tusome.

Emmanuel Kachele said...

Ni kweli kabisa Mwanammuni.Wasome wengi ndio hatuna utamaduni wa kusoma vitabu. Hata mimi nina mifano inayoishi kabisa. Kazini kwangu, na hata kwingineko, hali ya kujisomea ni tete. Na sio tu kujisomea, bali pia hata kuandika. Kuandika na kusoma ni skills ambazo huenda sambamba kama zilivyo skills za kusikiliza na kuongea.

Nataka nikujuze UKWELI kuhusu sisi Watanzania. Kwanza hatusomi, na ndio maana kila siku ukiona mtu ana Facebook account nyingine kwa mfano, basi ujue amesahau passowrd yake huyo. Na chanzo ni kwamba hatuna utamaduni wa kutunza diary. Na pili, kutokuwa na tabia ya kuandika ndiko kumetufanya tusiwe na tabia ya kujisomea pia. Hivi vitu vinaenda sambamba, nadhani hata Profesa Mbele anaweza kuwa na la kusema juu ya hilo siku moja.
Asante!

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...