Tuesday, April 26, 2011

Rais Obama Awasomea Watoto Hadithi


Leo, katika kuvinjari kwenye mtandao wa Facebook, nimeona video ya Rais Obama na familia yake. Wako bustanini wakiwasomea watoto hadithi.

Nimeguswa sana na video hii. Niliwahi kuandika makala kuhusu kuwasomea watoto vitabu. Katika makala hii nilielezea jinsi wenzetu huku Marekani wanavyojali suala hili, kuanzia watu wa kawaida hadi viongozi wa juu kabisa. Hata dakika ile Marekani iliposhambuliwa, tarehe 11 Septemba, 2001, Rais Bush alikuwa darasani na watoto wakisoma kitabu.

Makala yangu ile niliipanua na kuiboresha na imechapishwa katika kitabu cha CHANGAMOTO: Insha za Jamii. Katika makala hiyo, na kila mara ninapoongelea masuala ya aina hii ya kutokuwa na utamaduni huo kama wenzetu.

Lakini haingekuwa vigumu kuuanzisha na kuujenga utamaduni huo. Ni faraja kuona kuwa wako wengine wenye mawazo hayo hayo, na hapo napenda kumtaja Dada Sophie Kagambo Becker, ambaye ameelezea hayo katika blogu yake.

3 comments:

Anonymous said...

Maisha yanatofautiana Profesa kwasababu hivi sasa ninaweza nikatofautisha kutokea kwangu nilivokua shuleni na hapa nilipo.Mimi nilisomea shule za kawaida na sijalelewa na wazazi wangu ila shangazi alipenda kunichukua na kunipeleka mkoa mwingine na kanisomesha mpaka nimemaliza "form four".Lakini sikuwa na furaha kusema ule ukweli na sijajua kwanini baba yangu alimkubalia kwasababu akili yangu yote ilikuwa inaumia nakumkumbuka mama.Sio kwasababu ya matatizo ni kukaa mbali na baba na mama.Na hali hio ilinifanya nisiwe hata na hamu ya kusoma.Na kwakua hakuna mtu aliyekuwa ananitilia mkazo basi hali hiyo iliendelea mpaka namaliza la saba.Nikadhani nitachukuliwa na baba lakini alimuonea haya ndugu yake na shngazi alisema nikae nae na yeye ndie atatoa pesa za kunisomesha.Profesa mimi ni mtoto wa pekee na sina dada wala kaka.Sikupata elimu ya kueleweka nilipata "division 4"Hivi sasa natamani nirudi utoto ili nikapate elimu nzuri kitu ambacho hakiwezekani.Lakini Pro..Nilijaaliwa kuondoka na kuja uingereza kwa ajili ya kutafuta maisha na kwa bahati nikakutana na mwenzangu na tumeoana kwa miaka kumi sasa na watoto watatu.Maisha ya shule za huku ni tofauti na kwetu maana mzazi inabidi uingie ktk shughuli za kufundisha kusoma na kuandika na mambo mengi.Na ndio maana nikasema maisha yanatofautiana kwa sababu kwetu ni wazazi wachache ambao hujishughulisha na kuwapa suport ya kusoma watoto kama vile kumsomea mtoto "bed time story"au mtoto anaweza akakufata na kitabu umsomee na anafurahi kutokana na hadithi utakayo isoma.Kwa hiyo ni moja ya kumjengea kitabia cha kupenda kusoma hata ukipanda train watu utawaona wengi wanatembea na vitabu ili akiwa amekaa bure basi hujisomea angalau ansogeza muda ufike ashuke anakokwenda.Nimeipenda hii pro..

Mbele said...

Mdau anonymous, shukrani sana kwa mchango wako, ambao umenigusa sana. Nahisi utawagusa na wengine pia ulivyoelezea magumu ya utotoni.

Kinachovutia ni kuwa hukuruhusu magumu ya utotoni yawe kipingamizi cha kudumu kwa maisha yako ya baadaye. Na sasa umejaliwa kuishi mahali ambapo umepanua akili na kutambua kinachowezekana au kuhitajika kwa watoto wetu.

Tatizo la kule nyumbani ni kama ulivyoelezea, kwamba wazazi hawana mwamko wa kujumuika na watoto wao katika masomo ya hao watoto kama ilivyo huku ughaibuni. Hapa Marekani hali ni kama hiyo uliyoielezea. Mzazi unatakiwa ushughulike na kazi za masomo ambazo watoto wanapewa shuleni.

Tatizo jingine la nyumbani ni watu kuwa ni watu wa kutoa visingizio tu, na kutoa lawama kwa wengine, au kuilaumu serikali, badala ya kufanya juhudi kujisogeza mbele kwa hali yoyote.

Wa-Tanzania bado wanaendelea kutafuta nani wa kumlaumu, badala ya kujichunguza wao wenyewe na kuchukua hatua ya kujipeleka mbele.

Shukrani kwa mchango wako.

Sophie said...

Asante Prof.