Saturday, April 9, 2011

Hapa Kwetu: Akina "Anonymous" Sasa Ruksa

Tangu nilipoanzisha blogu yangu hii, sikupenda niruhusu akina anonymous kuchangia. Nilielezea duku duku zangu katika makala hii.

Lakini leo nimerekebisha mambo, kufuatia ombi la mdau mmoja ambalo amelitoa kwenye blogu ya Mwenyekiti Mjengwa. Nimeguswa na lugha ya kiungwana aliyotumia huyu anonymous. Kilichobaki sasa ni kuona hali itakavyokuwa.

5 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kuzuia anonymous kutoa mawazo yao mara nyingi huchukuliwa kama woga wa matusi na kukosolewa.
Kuna watu ambao si wastaarabu. Hutoa matusi lakini ukiwazoea unawaacha na hatimaye wanaacha utoto na kukua. Nakukaribisha kwenye ulimwengu mpya wa kutukanwa hata kusingiziwa. Muhimu inapaswa uvumilie. Maana hiyo ndiyo gharama ya demokrasia. Karibu tena kwenye ulimwengu wa ruksa.

Mbele said...

Huwa naandika kwenye blogu za wengine, ambako anonymous wanatukana. Kwa hivi, nimewazoea hao viumbe.

Sikuwa tayari kuwapa fursa hapa kwangu, kwa hoja kwamba kila mwenye hoja awe na ushujaa wa kujitambulisha kama ninavyofanya mimi popote.

Vile vile, niliona kwamba mtu kujitambulisha ni namna ya kuwaheshimu wasomaji.

Lakini katika kutafakari tena mtazamo wangu, nimekuja kupata wazo, ambalo limenivutia. Kufungua milango ili hata anonymous wasikike ni njia nzuri ya kutathmini hali halisi ya jamii yetu, uwezo wa kuelewa mambo, kufikiri, kujenga hoja, na kadhalika. Ni kioo cha kuiangalia jamii.

Simon Kitururu said...

Ila pamoja na uhuru mimi naweza kumshabikia anayetukana akiwa kajitambulisha jina kuliko ajifichaye. Ila nakumbuka pia matusi mengine yanalugha tamu na ni mpaka mtu afikirie ndio anaweza kujua lisemwalo ni tusi !:-(

Mbele said...

Baada ya kuwaruhusu akina anonymous, nimeona uchangiaji unaongezeka kwenye blogu yangu. Kumbe anonymous wengine ni vichwa kweli :-)

Anonymous said...

Naomba nikutoe wasiwasi kabisa Pr. Mbele. Anonymous ni binadamu wala huhitaji kufikiri kuwa ni Virus fulani. Kumbuka binadamu tuna imani, tabia na tamaduni tofauti. Uliandika kitabu fulani "Africans Americans in cultures" nimependa mahali fulani uliposema Mmarekani hawezi kushirikiana na yeyote popote hata kwenye Dinner mpaka kwanza amejitambulisha. Sisi Watanzania ni tofauti, kujitambulisha sio silika yetu hata kidogo, tunapanda basi moja bila hata kujuana majina. Tunaweza kula pamoja bila kujuana, Wewe nadhani ulianza kuiga tabia ya kimarekani huko Minnesota kutaka kila mmoja ajitambulishe jina kwenye Blog yako. Wamarekani hawaminiani wao kwa wao ndio maana kila saa wanajitambulisha majina, na huo ni utumwa mkubwa sana. We Africans are communal and social people, we trust to each other,and don't fear for strangers. Sisi akina Anonymous tutakusaidia wewe kukumbana na Challenge mbalimbali,unataka majina yetu ya nini? Je unapokuwa kwenu Ludewa au Namtumbo misibani au kwenye arusi unajitambulisha jina? Nakulaumu sana kufunga uhuru wa watu kwa muda mrefu. Anyway nakupongeza japo umechelewa sana kufungua.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...