Katika matamasha ya aina hiyo, hasa ya vitabu, navutiwa ninapowaona wazazi wamekuja na watoto wao. Huku Marekani ni jambo la kawaida. Katika tamasha hilo la elimu na ajira Dar es Salaam, nilimwona mama mmoja amekuja na mtoto wake. Mama huyu, anayeonekana katika picha hii, alikuja kwenye kibanda changu, ambapo nilikuwa nimeweka vitabu vyangu, akaniuliza masuali kadhaa, huku mwanawe akisikiliza. Niliongelea masuali yake, kuhusu shughuli zangu katika elimu na uandishi, na kadhalika. Ilikuwa ni fursa kwangu pia ya kumhamasisha mtoto wake. Sitasahau mfano alioonyesha mama huyu. Wahenga walisema, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
No comments:
Post a Comment