Tuesday, April 5, 2011

Mwalimu Nyerere Aongelea Uongozi, 1995

Suala la uongozi lilikuwa moja ya vipaumbele vya Mwalimu Nyerere maisha yake yote. Tunasikia, kwa mfano, jinsi alivyolichukulia suala hili alipokuwa kiongozi wa wanafunzi katika shule ya Tabora. Wakati wa kupigania Uhuru na baada ya Uhuru aliliongelea suala hili tena na tena, kama vile katika "Azimio la Arusha" na "Mwongozo."

Mwalimu aliliongelea suala hili tena, kwa masikitiko, katika kitabu chake cha "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania," akiihofia hatima ya Tanzania kutokana na uongozi mbovu wa CCM. Niligusia suala hilo katika makala hii hapa. Hata baada ya kuandika kitabu hiki, Mwalimu aliendelea kuongelea suala la uongozi. Hebu msikilize katika hotuba yake hii ya mwaka 1995.

2 comments:

emuthree said...

Ndio profesa, umenikumbusha enzi za huyu mzee wetu muhimu sana,...naona hotuba zake wanaziweka kwenye televisheni, halafu ikifika siku ya kumbukumbu yake ni matanuzi na....lakini `matendo' hayazihirishi hivyo...hii tutaiita nini! Nashangaa sio nauliza!

Mbele said...

Kuhusu Mwalimu Nyerere, CCM wanafurukuta sana kufanya usanii. Kwa upande moja, hawana ubavu wa kumsahau kabisa, kwani wengi wetu bado tunamkumbuka, na tunamheshimu kama Baba wa Taifa na mchango wake mkubwa.

Kwa hivyo, utawasikia hao wanaoitwa viongozi wa CCM wakikumbushia kuwa Mwalimu alituachia amani. Kwa mfano, katika mazingira haya ya sasa ya maandamano ya CHADEMA, nimeshawasikia hao CCM wakimtaja Mwalimu na kudai kuwa hao wanaoandamana wanataka kutuharibia amani aliyotuachia Mwalimu.

Kwa upande wa pili, hao CCM hutawasikia wakielezea mengine ambayo Mwalimu huyo huyo aliyataka, kama vile kujenga jamii ya usawa, kuwa kuhakikisha mali ya Taifa inatumika kwa manufaa ya wananchi, kutokomeza unyonyaji, na kupambana na mfumo wa ubepari, ambao umejikita ndani ya nchi na ni sehemu ya mfumo wa ubepari wa kimataifa.

Hayo hao CCM hawayataji, kwani yanapingana moja kwa moja na ufisadi ambao CCM imeukumbatia. CCM wanafanikiwa kwa kiasi cha kutosha katika huu usanii, kwa sababu wananchi ni wavivu ambao hawasomi wala kufuatilia mafundisho ya Mwalimu.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...