Jana, tarehe 5 Oktoba, jioni, nilihutubia mkutano ulioandaliwa na vyuo vikuu viwili vya Colombia, Amerika ya Kusini. Mada yangu ilikuwa "Culture and Business: a Broad Perspective From Africa to. Latin America."
Kwa zaidi ya mwaka, mada ya utamaduni na biashara imenivutia. Nilipoanza kuipenda, niliandika "Culture and Business Between Africans and Americans." Halafu, nilihutubia Trade With Africa Business Summit nikiwa nimealikwa kuongelea kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences.
Hatimaye sasa, nilipopata mwaliko kutoka Colombia, nilijikuta niko tayari kutosha. Kasoro pekee ilikuwa kwamba sikuufahamu utamaduni wa Amerika ya Kusini kama ninavyoufahamu ule wa Afrika na Marekani. Kwa hiyo, nilijielimisha kiasi kabla ya siku ya mkutano.
Nilijifunza mengi ya msingi, ambayo yalinifanya nitamke na kusisitiza mkutanoni kwamba utamaduni wa Amerika ya Kusini unafanana kiasi kikubwa na ule wa Afrika. Kwa hiyo, biashara baina ya pande hizi mbili itakuwa rahisi. Nilitoa angalizo kuwa itabidi kuzingatia tofauti za lughha zilizopo katika hizi pande mbili za dunia, ili kuleta uangalifu katika mawasiliano, utangazaji wa biashara, na kadhalika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
No comments:
Post a Comment