Mimi kama mwandishi, ninakumbuka juhudi ninayofanya na taabu ninayopata katika kuandika vitabu. Kitabu cha Matengo Folktales, kwa mfano, kilichukua miaka yapata 23 kukiandaa, yaani tangu kurekodi hadithi, kazi yenye usumbufu mwingi, kuzitafsiri, kurekebisha tafsiri tena na tena, tena na tena, halafu kuziandikia uchambuzi, na kurekebisha tena na tena, huku nikifanya utafiti maktabani juu ya mada ya hadithi za jadi, ili niweze kuchambua hadithi zilizomo kitabuni kwa upeo unaofaa katika kufundishia vyuoni, na kadhalika.
Nilijikuta nikitafakari mambo mengi ya aina hiyo, wakati mwingine nakwama kabisa, halafu baada ya muda najikongoja tena, hivi hivi, na baada ya miaka yapata 23 ndio nikachapisha "Matengo Folktales."
Kitabu cha Chickens in the Bus: More Thoughts on Cultural Differences, ingawa ni kidogo sana, kurasa 43 tu, nacho kilinichukua yapata miaka 15 kukiandaa. Nilipigika na kuchakarika. Lakini baada ya kuchapisha, najiona mwenye faraja kubwa na ushindi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
No comments:
Post a Comment