Friday, September 10, 2010

Upatikanaji wa Vitabu Vyangu

Kutokana na maulizo ya wadau, napenda kutangaza kuwa vitabu vyangu vinapatikana Tanzania, sehemu zifuatazo:

Arusha (Kimahama Literature Center)
0786242222

Dar es Salaam (Sinza)
0754 888 647
0717 413 073

Bagamoyo
0754445956

Karatu (Bougainvillea Lodge)
0754576783

Longido (Cultural Tourism Program)
0787855185

Mto wa Mbu (Cultural Tourism Program)
0786373099

Walioko ughaibuni wanaweza kuvipata sehemu hizi:

Duka la mtandaoni, Bofya hapa

St. Olaf College Bookstore, Fax 507 786 3779, simu 1-888-232-6523

Africonexion (info@africonexion.com, simu 507 403 9756)

4 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mimi nitaagiza viwili hivi karibuni. Visaasili vya Kimatengo na kile cha Utamaduni. Kazi nzuri Prof.

Mbele said...

Mwalimu Matondo, shukrani kwa ujumbe wako. Nashukuru kwa kutuongezea msamiati sisi ambao hatukuwa tunajua hilo neno "visaasili." Ni neno muafaka kabisa, kwa kuzingatia ufahamu wangu wa taaluma hii iitwayo "Folklore" kwa ki-Ingereza.

Vitabu hivi naweza kukuletea muda wowote, ukitaka, maana sikosi nakala.
Narudia shukrani.

Unknown said...

Na mimi pia najipanga na kile kitabu cha matengo folkrole,nafkil ndo itakuwa field yangu,napenda sana.

Mbele said...

Ndugu Mlengela, ukijibanabana ukakipata kitabu hiki, utakuwa hujateleza, iwapo unapenda somo hili.

Huku Marekani kinatumika kwenye masomo vyuoni. Walimu kadhaa katika vyuo vikuu vya Tanzania nao wanakitumia, na maandishi yangu mengine..

Nilitumia miaka yapata 23 kukiandaa kitabu hiki, yaani tangu kurekodi hadithi zilizomo, kuzitafsiri, na kuziandikia uchambuzi.

Kitabu hiki, ingawa ni cha ukubwa wa wastani tu, kimebeba yale ya msingi ninayofundisha katika somo hili la visaasili.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...