Thursday, June 16, 2011

Migongano ya Utamaduni wa wa-Marekani na Wa-Afrika

Nimealikwa na umoja wa watu wenye asili ya Afrika hapa Minnesota kuongoza mjadala, tarehe 18 Juni, keshokutwa, kuhusu matatizo yanayowakabili wa-Afrika hapa Marekani yatokanayo na tofauti za tamaduni. Umoja huo unawajumuisha wa-Afrika wanaoishi hapa Marekani, wa-Marekani Weusi, na watu wenye asili ya Afrika watokao Amerika ya Kusini, visiwa vya Caribbean, na kadhalika.

Taarifa kamili za mkutano ni hizi:

MAHALI PA KUKUTANIA:

Center for Families
3333 North 4th Street
Minneapolis, Minnesota

MUDA:

Juni 18, 2011. Saa 6-8 mchana.

Hakuna ki-Ingilio, na wote mnakaribishwa. Nangojea kwa hamu kwenda kuongoza mjadala huu muhimu kwa jamii.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni jambo la busara sana ningekuwa karibu hakika ningehudhuria maana inaonekana kutakuwa na mjadala kiboko kwelikweli....tunasubiri hapa hapa kibarazani ....

Mbele said...

Shukrani kwa ujumbe wako wa kutia moyo. Tutajitahidi.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...