
Kati ya mambo yaliyonifanya niandike kitabu hiki ni kukidhi mahitaji ya wa-Marekani wanaoenda Afrika kwa sababu mbali mbali, kama vile masomo, utafiti, utalii na shughuli za kujitolea. Kilihitajika kitabu cha kuwaelewesha mambo ya msingi yanayotufautisha utamaduni wao na ule wa wa-Afrika.
Msimamo wangu ni kuwa pamoja na tofauti zilizopo miongoni mwa wa-Afrika wenyewe, na pamoja na tofauti zilizomo miongoni mwa wa-Marekani, kuna kitu tunachoweza kukiita utamaduni wa mw-Afrika, na kuna kitu tunachoweza kukiita utamaduni wa m-Marekani. Katika kuandika na kuongelea masuala hayo, najaribu kuthibitisha jambo hilo. Nafarijika kuwa juhudi hizi zinakubalika na watalaam na wadau kama hao wa Dartmouth Alumni.
2 comments:
Hongera Profrsa kwa kitabu hicho kinacho onyesha umahili na ufundi wa uandikaji wa vitabu kwa lengo la kuelimisha jamii kwa ujumla.
Kazi ya uandishi siyo rahisi,nakama Taifa lingewajali watunzi na waandishi wa vitabu vya taaluma,vya kufundishia na jujifunzia naimani uhaba wa vitabu vya ziada na kiada usingekuwepo katika shule la vyuo vyetu.
Kazi yako inaonekana hasa katika picha mlizopiga na wanataaluma wenzako wa uandishi.Nakutakia kazi njem katika kazi hii muhimu.
Shukrani kwa ujumbe. Nafarijika kuwa kitabu hiki kinatoa mchango kwa wenye kutambua mahitaji yao. Kwa huku Marekani, hili liko wazi. Kwa upande wa Tanzania, napenda kuitaja kampuni ya J.M. Tours ya Arusha, inayomilikiwa na mama mzungu ambaye ameolewa na Mtanzania. Mama huyu alipokisoma kitabu hiki, miaka kadhaa iliyopita, alianza kukipigia debe, na kwanza alihakikisha kuwa wafanya kazi wake wanakisoma. Leo, madreva wa J.M Tours ukiwaulizia, watakuambia jinsi kitabu hiki kinavyorahisisha majukumu ya kushughulika na watalii.
Kampuni ya aina hii ni kampuni iliyoamka. Imejiweka sawa katika ushindani wa utandawazi wa leo, unaotegemea elimu, ujuzi, na maarifa.
Post a Comment