Sunday, January 19, 2014

Vitabu Ulivyonunua au Kusoma Mwaka 2013

Mwaka ni muda mrefu. Hata mwezi ni muda mrefu. Tafakari uliutumiaje mwaka 2013. Uliitumia fursa ile kwa kujiendeleza? Ulijiongezea ujuzi na maarifa katika fani yoyote?

Ulisoma vitabu? Kama una watoto, uliwanunulia vitabu? Kama hukufanya hivyo, wewe una matatizo, wala usijidanganye.

Kama wewe ni mnywaji wa bia, unadhani ulitumia fedha kiasi gani kwa unywaji huo, kwa wiki, mwezi au kwa mwaka? Utasema hukuwa na hela ya kununulia vitabu?

Kuna maktaba katika miji mingi, wilayani na mikoani. Baadhi nimezitembelea na kuandika ripoti zake katika blogu zangu, miji kama Lushoto, Mbulu, Karatu, Dar es Salaam, Mbinga, Moshi, Iringa na Songea. Je, mwaka 2013 uliingia humo? Mara ngapi, na ulisoma vitabu vipi?

5 comments:

Unknown said...

Sadly enough Doc there are so many of us who have taken the bait, not only do we not read we do not research or cross check data ....simply because it is current "Gossip" or a wives tale that "they or everybody" says . Feelings have been influenced and the details are too complicated, after they have been trained & certified by a group who at best has taken a financial advantage of them , there is not a place for individuals to make true sense of the world and it is not that the information is there it is that the sources are not in cannon and it challenges "The status Quo " this means that he who knew them at the top are many times caught in cultural lag but are able to treat those from their circle to oppression so that they get oppressed and defeated by folks from the same oppressive group who claim that they are not opposing you, history teaches that the outlier is the empowerment of the uprising of a group and it keeps the group ahead of the learning curve hence, the wise question everything under God and faith has its basis in what is genuine and that is about us being current on ideas and information

Anonymous said...

Prof. kampeni zako za kusoma vitabu ni nzuri sana ila wengi wetu tuna "allergy "ya fani hiyo.

Bahati mbaya sijaona email yako kuna jambo nilitaka nikunong'oneze.

Mbele said...

Anonymous, shukrani kwa ujumbe wako. Anwani yangu ni info@africonexion.com

Anonymous said...

Nashukuru Prof. kwa email, nitakunong'oneza punde.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Laiti watanzania na hata waafrika wangekuwa wanaona vitabu kama zana za ukombozi kama aonavyo kaka Mbele huenda tungesonga mbele. Mwenzenu mwaka jana nilisoma si chini ya vitabu 30 kikubwa kikiwa cha rafiki yangu profesa Hans Werner cha "The Constructed Mennonite" aliyenipa mwenyewe baada ya kuwa namsumbua kuhusu mswaada wake. Pia nilirudia kitabu nilichotumiwa na rafiki yangu Attilio Tagalile cha "Endless Toil." Mbali na vitabu vya kawaida, nilisoma article nyingi juu ya dini za kibuddha, jaini na nyingine nyingi. Nilisoma pia uchambuzi wa Bhagavad Gita na Mahabharata na madude mengine mengi. Kwa sasa nipo nasoma rasimu ya katiba mpya ya Tanzania. Nimeandika makala zaidi ya 100 ukiachia mbali kuandika miswaada miwii huku mmmoja wa kitabu cha watoto ukiwa wa tatu tukiandika na mke wangu na tunategemea kitabu hicho kutoka hivi karibuni kama mchapishaji atatimiza ahadi yake. Habari mbaya ni kwamba Kitabu change cha NYUMA YA PAZIA kimeendelea kudoda baada ya wachapishaji kusema kuwa hawawezi kukichapisha kwa kuogopa ku-Kolimbwa.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...