Saturday, January 25, 2014

Wiki Mbili Zijazo Kitabu Hiki Kinatimiza Miaka Tisa Tangu Kichapishwe

Wiki mbili tu kuanzia sasa, kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences kitatimiza miaka tisa tangu kichapishwe.

Sitaiacha siku hiyo ipite hivi hivi. Nawazia nini cha kufanya. Labda nitaandika ripoti kadhaa juu ya mafanikio yake. Kitabu hiki sikukiandika kwa ajili ya kujipatia pesa, ingawa kimeniletea pesa, tena sio chache.

Lengo langu na mafanikio yangu makubwa yamekuwa katika kuwagusa na kuwasaidia watu. Katika hilo najivunia kazi ngumu niliyofanya katika utafiti na uandishi wake.

Wako wachache ambao wamekuwa wakiniletea kejeli. Hao nawaona kama watu wasio na akili timamu. Kinachoudhi ni kuwa watu hao wanaongelea kitabu ambacho hawajakisoma.

Sitaweza kuleta maoni ya wote waliokisoma wakanipa maoni yao. Hao ni watu makini. Nawashukuru.

2 comments:

Anonymous said...

Prof wakati mwingine unanichanganya. Kwani wanaokukejeli hawana haki ya kuwaza wawazavyo na kusema waonavyo au unataka uungwe mkono hata pasipostahili?
Kitabu kimoja imekuwa nongwa. Je ungekuwa umeandika vingi ingekuwaje? Kweli Subhanna anatujua waja wake. Yumkini mtu mwenye majivuno kama wewe ungepewa vipaji vya kuandika mambo makubwa kama maprofesa kama vile Ngugi, Mazrui, Soyinka na wengine si ingekuwa taabu. Ingawa sijawahi kuandika kitabu, mwalimu wangu alinifundisha kuwa ukishaandika kitabu kinaacha kuwa mali yako bali mali ya wasomaji ambao wana haki ya kukuhukumu watakavyo. Najua utaniwakia. Sitaajali kwa vile najaribu kufaidi haki yangu ya kutoa maoni yangu. Prof huna haja ya kuwaita watu hamnazo kana kwamba wewe unajijua kuliko wao. Kama wamekandia kitabu chako si unaachana nao badala ya kuwa nongwa? Kwa leo yangu ni hayo.

Mbele said...

Hawana haki hata chembe kwa sababu.moja. Hawajakisoma hiki kitabu.Je wewe unatetea upumbavu huo.?

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...