Nimejifunza mengi katika kutembelea nyumba hii. Nilipoingia, nilijumuika na wageni wengine wanne, tukafanya ziara pamoja, tukiongozwa na dada aliyejitambulisha kwa jina la Michelle ambaye anaonekana pichani.

Alituelezea mambo muhimu yaliyomlea Ernest Hemingway katika nyumba hii. Mfano ni namna mama yake alivyotaka kila mtoto na mtu mwingine katika nyumba hii awe na ujuzi wa muziki. Kabla ya ziara hii, nilijua kuwa mama yake Ernest Hemingway alitaka Ernest ajifunze muziki, lakini sikujua kuwa alitaka hivyo kwa kila mtoto na wengine pia. Ziara hii pia imenifungua macho kuhusu namna mtindo wa usimuliaji hadithi aliokuwa akitumia Ernest Hemingway ulivyojengeka tangu utoto wake katika nyumba hii.
No comments:
Post a Comment