Monday, June 19, 2017

Mzalendo Tundu Lissu Aliyasema Haya Mambo

Leo nimeona taarifa za kufikishwa mahakamani watuhumiwa wakuu wawili wa ufisadi mkubwa nchini Tanzania. Watuhumiwa hao ni Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira. Wananchi wengi tunalichukulia jambo hili kama mwendelezo wa juhudi za Rais Magufuli kusafisha nchi. Lakini kitu kimoja kinachonikera ni jinsi watu wengine wanavyojaribu kupindisha historia ya suala hili. Hapa naleta hotuba ya Tundu Lissu aliyoitoa Bungeni kabla ya ujio wa Rais Magufuli.

2 comments:

Emmanuel Kachele said...

Elimu ndogo ya Watanzania wengi ndio mtaji wa Wanasiasa wa Awamu hii. Kama elimu ingetolewa kwa watu basi hali ingekuwa tofauti. Kila mara mimi naamini kuwa 'Wapiga Kura Walioelimika ndio huleta viongozi bora au ndio hulifanya taifa lipige hatua stahiki za maendeleo'.
Unaweza ukashtuka kwa kuyaona haya, lakini ukienda vijijini unaweza kuzimia: Wananchi hawajui chochote; wao ni wapiga makofi tu, na hasa ukizingatia Watanzania na kusoma ni sawa na 'Mpanda ngazi na mshuka ngazi, kamwe hawawezi kushikana mikono!

Mbele said...

Ndugu Emmanuel Kachele, shukrani kwa ujumbe wako. Dalili moja ya ujinga uliopo ni jinsi watu wanavyomlalamikia au kumshambulia Tundu Lissu eti anapinga kila kitu. Kutoa mawazo na kujieleza ni haki ya kila binadamu, ambayo imetambuliwa katika tangazo la kimataifa la haki za binadamu na imetambuliwa katika katiba ya Tanzania. Tundu Lissu anatumia haki yake, na wala hawazuii watu kujibu au kupinga hoja zake. Badala ya kulalamika, watu wajibu hoja. Watu wenye akili hufanya hivyo.

Kama Tundu Lissu hakubaliani na yale wanayosema wengine, akiwemo rais, na anapinga muda wote, tatizo liko wapi? Masuala yenyewe ni hayo yanayohusu maslahi ya Taifa. Kila raia anayeipenda nchi yake na kuitakia mema, anawajibika kutoa mchango wake. Mawazo ni mchango mmoja wapo. Na hiki ndicho Tundu Lissu anachofanya. Akae kimya kwa nini? Hata mimi sikai kimya ninapoona suala la maslahi ya nchi yangu linapelekwa kusikotakiwa.

Ujinga unasababisha watu wasitambue kuwa anavyofanya Tundu Lissu anatoa changamoto ya kuwafanya watu wafikiri nje ya upeo waliozoea au nje ya upeo wanaouwazia wao. Elimu haisongi mbele kama hakuna watu wachochezi wa fikra kama Tundu Lissu. Watu wanaopinga fikra zinazokubalika na jamii wanaipa jamii fursa ya kufungua milango mipya ya fikra.

Mimi kama mwalimu ninawajibika kuwalea vijana wawe watu wa kuhoji mambo bila ukomo. Vinginevyo, kuna sababu gani ya kuwa na vyuo na kusema kuwa tunaelimisha? Kwa maana hiyo, kwa kuwa ninaelewa kuwa elimu ni msingi muhimu wa maisha na maendeleo, ninamwona Tundu Lissu kama mtu muhimu kwa maendeleo ya nchi, na ni mfano wa kuigwa.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...