Saturday, June 27, 2009

Makala ya "Kwanza Jamii" Yachapishwa Marekani

Wiki kadhaa zilizopita, nilipata mwaliko kutoka kwa Ndugu Maggid Mjengwa, kuwa niandike makala katika gazeti lake jipya la Kwanza Jamii. Nilikubali, na niliandika makala ya kwanza yenye kichwa "Maendeleo ni Nini?." Makala hii ilichapishwa mwezi Aprili, 2009.

Siku moja, katika maongezi na Mmarekani Mweusi mmoja katika mji wa Minneapolis, nilimwambia kuwa nimeanza kuandika makala za kiSwahili katika gazeti moja la nyumbani Tanzania. Kwa vile alikuwa na duku duku ya kujua zaidi kuhusu makala hizo, nilimweleza kuhusu makala yangu hiyo ya kwanza. Huyu Mmarekani tulikuwa tumefahamiana kwa wiki kadhaa, tukiwa katika shughuli za kuandaa tamasha la utamaduni wa kiAfrika, liitwalo Afrifest.

Alivutiwa na mada na mtazamo wa makala, akasema ingefaa kuchapishwa katika gazeti la mtandaoni ambalo yeye na watu wengine walikuwa wanaliandaa. Alisema kuwa mawazo niliyoandika kuhusu maendeleo yatawafaa watu wa Marekani pia, kama vile waMarekani Weusi, ambao nao wamepitia msukosuko wa kutawaliwa kimawazo, kama waAfrika.

Tulikubaliana niitafsiri, na kisha imechapishwa katika gazeti hilo liitwalo TheUrbanFly.

7 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Heshima kwako Profesa.
Naamini juhudi nyingi hulipa japo wakati mwingine huonekana kama inachukua muda mrefu kabla malipo hayajaonekana.
Lakini napenda kukuhakishia kuwa ELIMU YAKO INAFANYA KAZI HASA KWA SISI AMBAO TUNAJIFUNZA MENGI KUTOKANA NA KUSOMA NA KUJITAHIDI KUIFANYIA KAZI.
Baraka kwako na mafanikio mema Profesa

Mbele said...

Mzee wa Changamoto

Shukrani.

Elimu haina mwisho, na mimi huwa najitahidi kujielimisha kwa bidii kuliko hata wakati nilipokuwa mwanafunzi wa shahada za juu.

Ni mapambano na adui ujinga, mapambano ambayo, tukizembea, adui huyu ni mwepesi kutuelemea.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...
This comment has been removed by the author.
Simon Kitururu said...

Mliotangulia mmemaliza lakini na mimi nataka kukiri ni miongoni mwa WAJIFUNZAO mengi kutoka kwenye kazi za Prof. Mbele.

mumyhery said...

Kazi nzuri sana Mkuu, na ni kweli kabisa elimu haina mwisho ila sisi tunajisahau na ni wepesi wa kuridhika kuona hapa sasa panatosha hasa tukipata ajira tu basi

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sijuui sana mambo ya kusifia lakini kwa mzee km wewe kujichanganya na mayanki online ni ishara nzuri ya kuleta mapinduzi chanya juu ya matumizi ya net kwa vjana.

nakufwagiliya mzee

Yasinta Ngonyani said...

Mimi nasema pia elimu haina mwisho na mimi ni mmoja wa wale wanaojifunza mengi kutoka kwako Pro.Mbele. Ubarikiwe sana.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...