Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
2 comments:
Sera ya lugha ya Tanzania ni moja kati ya sera za lugha za kuchekesha kabisa duniani. Baada ya mikakati ya kukifanya Kiswahili kuwa elimu ya kufundishia elimu ya juu (kuanzia sekondari na kuendelea) kukwama, sera hiyo imeshapitwa na wakati na imebakia kuwa sera ya undumilakuwili mno - huku haiko na huku haiko. Sijui inamsaidia nani! Mtoto anamaliza darasa la saba hajui hata kujitambulisha kwa Kiingereza halafu kimiujizaujiza tu anategemewa awe ameshafahamu Kiingereza anapoingia fomu wani kiasi cha kuzimudu sawasawa "Newton's Laws of Motion". Kuanzia hapo elimu inakosa maana na inageuka kuwa mchezo wa kukariri tu na kama huwezi kukariri basi umekwisha. Kwa walioko mijini na ambao wazazi wao wana uwezo wa kuwapeleka Academy (ambazo ziko kila kona) basi wana unafuu lakini kwa watoto wa kijijini (ambao kwa bahati mbaya ndiyo wengi), ni giza tupu! Sera hii ya lugha ni kiinimacho na inahitaji kubadilishwa kwa manufaa ya kila Mtanzania.
Hayo unayoeleza yanasikitisha. Kingine kinachosikitisha ni uzembe wa wananchi katika matumizi ya lugha, uzembe kama huu wa huyu kigogo kwenye katuni.
Huyu kigogo ana wajibu wa kuongea kiSwahili sahihi. Lakini waTanzania wakishasoma kiIngereza kidogo, wanafanya kila jitihada kukichanganya humo kwenye kiSwahili. Kuna tatizo kubwa hapa ambalo watalaam wa isimu jamii na saikolojia wanaweza kuandikia hata vitabu.
Binafsi, pamoja na kuwa mwalimu wa kiIngereza, niliamua miaka mingi iliyopita kufanya juhudi kuandika kiSwahili pia. Ndio maana ninaandika kwenye gazeti la Kwanza Jamii. Ni namna ya kupima uwezo wangu wa kutumia lugha hii, na pia kutoa mfano kwa watu kama huyu kigogo kwenye katuni, ambao naamini wana matatizo kichwani.
Post a Comment