Wednesday, February 21, 2018

Maana ya Uzalendo

Kwa kuzingatia jinsi dhana ya uzalendo inavyovurugwa na watu mbali mbali, nimeona nilete tamko la Ilhan Omar, Msomali Mmarekani ambaye ameweka historia hapa Marekani kwa kuchaguliwa kuwa mwakilishi katika bunge la jimbo la Minnesota. Anafafanua kwa lugha rahisi maana ya uzalendo. Anachosema ni kuwa uzalendo si kutetea uongozi au kiongozi wa nchi, bali ni kutetea na kuzingatia maslahi ya nchi, katiba yake, na watu wake. Anasema ni kosa kufikiri kwamba mkuu wa nchi asikosolewe. Anasema kwamba katika nchi ya kidemokrasia, na katiba inayotambua uhuru wa watu kutoa mawazo na kujieleza, watu wana haki ya kumkosoa mkuu wa nchi, kumshinikiza afanye mambo ya manufaa, na kumwajibisha, bila wasi wasi au woga wa kueleweka kwamba si wazalendo.

2 comments:

Emmanuel Kachele said...

This is a very good lesson for understanding what patriotism is all about. I wish all Tanzanians had this in their minds including leaders!
Thanks you Professor!

Unknown said...

Ahsante sana profesa kwa hili.Ni vema makala yako hii ukaibandika kwenye ukurasa wako wa facebook ili watanzania wengi wapate ujumbe huu.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...