
Hii si shughuli ya kwenda kusimulia hadithi tu. Ni kuelimisha kuhusu misingi, maana, na dhima ya hadithi za jadi katika utamaduni wa Afrika. Jadi ya kusimulia hadithi ni sanaa yenye kugusa vionjo na hisia za binadamu, pia ni nia ya kuhifadhi elimu na kuelimisha. Hadithi zinayotafakari maisha, tabia na mahusiano ya binadamu, na masuala ya maadili.
Hadithi zimefungamana na aina zingine za sanaa ya maneno kama vile methali na nyimbo. pia zimefungamana na mila, desturĂ, na imani. Ni kioo cha jamii, lakini pia ni kichocheo cha mwenendo wa jamii. Upana huo wa mtazamo kuhusu hadithi nimeubainisha katika kitabu changu, Matengo Folktales ambacho kina hadithi kumi, pamoja na uchambuzi wangu wa kila hadithi. Pia kina insha juu ya padithi kwa mtazamo wa kitaaluma, lakini kwa lugha rahisi.
Mhadhara wangu wa Red Wing utaelimisha kuhusu mchango wa wa-Afrika katika utamaduni wa ulimwengu. Nitaelezea kuwa sanaa ya usimuliaji hadithi ilianzia Afrika, sambamba na kutokea kwa binadamu na lugha. Nitaelezea kuwa falsafa haikuanzia Ulaya, kwa akina Socrates na Plato, bali ilikuwepo Afrika, katika hadithi na aina nyingine za fasihi simulizi. Mafundisho ya hadithi na fasihi simulizi kwa ujumla kuhusu maisha na mahusiano ya binadamu bado yana maana na umuhimu
katika ulimwengu wa leo na kesho.
Ninatoa shukrani kwa uongozi wa Red Wing Public Library na Goodhue County Historical Society kwa kunialika kwenda kutoa mhadhara huu. Nafurahi pia kuwa sitaenda kuzungumza tu, bali pia, k kuoutakuwa na shughuli ya watu kununua na kusainiwa kusaini vitabu vyangu. Vitabu vitadumisha ujumbe wangu katika maisha ya watakaovisoma.
No comments:
Post a Comment