Friday, February 16, 2018

Mrejesho Kuhusu Kitabu

Ni furaha na faraja kwangu kama mwandishi kupata mrejesho kutoka kwa wasomaji. Leo asubuhi, nilipoamka, niliona ujumbe kutoka kwa mwalimu wa chuo cha St. Lawrence. Ameandika:

Mimi ni ndugu Kitito. Tulikuwa wageni wako katika kongamano la African network. Mimi na Robin tunashukuru mno kwa kitabu chako "Africans and Americans." Tunakitumia darasani mwetu. Wanafunzi wamefaidika mno...

Huyu mwalimu Robin anayetajwa nilishaandika habari zake katika blogu hii. Baada ya mimi kusoma ujumbe wake, mwalimu Kitito amenipigia simu, akanielezea zaidi kuhusu kitabu kinavyotumiwa. Nami nilimwelezea nilivyokiandika, baada ya miaka mingi ya kukabiliana na maisha ya Marekani. Nilimweleza kwa nini nilitumia mtindo ambao si kawaida kwa wanataaluma.

Nimefarijika kupata mrejesho kutoka kwa waalimu hao ambao wanatumia kitabu changu, nami nimeona niweke kumbukumbu hii hapa, kama ilivyo kawaida yangu.

No comments:

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...