Napenda kuwafahamisha wasomaji wa blogu hii na maandishi yangu mbali mbali kuwa nimejiunga "twitter," mtandao wa mawasiliano ya haraka haraka. Bofya hapa.
Shukrani kwa kuwa pamoja nami katika blogu hii. Nawakaribisha kujumuika nami "twitter" vile vile na kufuatilia shughuli zangu kwa karibu zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
3 comments:
Hii "twitter" mbona kizungumkuti! Tekinolojia zinakwenda kwa kasi ajabu na inabidi kuwa ngangari. Baada ya kuwa nimekufuatilia na kujifunza vya kutosha kuhusu ku"twita" basi pengine nami nitaijaribu...Kazi kweli kweli.
Haya mambo ni mageni kwangu pia, lakini najikongoja. Faida moja ninayoiona ni ya kupata taarifa mbali mbali, maadam uwe umechagua washiriki unaowaona wanaweza kukupanua mawazo.
Mwanzoni nilidhani hizi kumbi kama twitter ni za vijana wadogo wa siku hizi, kumbe nimeona kuwa huko kuna watu maarufu, makampuni, na taasisi mbali mbali. Ni sehemu nzuri ya kutangaza shughuli mbali mbali.
TARATIBU PROFESA utafika tuuuuuuu, kizazi kipya hiki
Post a Comment