Thursday, January 13, 2011

Nimejiunga na Bodi ya Operation Bootstrap Africa

Nimerejea jioni hii kutoka Minneapolis, kuhudhuria mkutano wa bodi ya Operation Bootstrap Africa (OBA). Mimi ni mwanabodi wapya. Niliteuliwa mwishoni mwa mwaka jana, na mkutano wa leo ulikuwa ni wa kwanza kwangu.

Nilifahamu habari za OBA tangu nilipokuwa nasoma Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, 1980-86, kwamba ilikuwa inajishughulisha sana na masuala ya elimu Tanzania. Mwaka jana, nilipopendekezwa kuwa mwanabodi, nilifanya juhudi za kuifahamu zaidi OBA.

OBA, imefanya mengi ya manufaa kwa nchi ya Tanzania, kwa kuhamasisha michango miongoni mwa wa-Marekani. Yeyote anayewafahamu vizuri wa-Marekani, anatambua jinsi wanavyojituma katika shughuli za kujitolea. Ni jambo ambalo wanafundishwa tangu utotoni, na linasisitizwa mashuleni, kuanzia madarasa ya mwanzo kabisa hadi chuo kikuu.

Nilikaa katika mkutano wa leo nikisikiliza taarifa za michango inayotolewa na watu mbali mbali kwa manufaa ya Tanzania, watu wenye hela nyingi na wasio na hela nyingi, nikawa najiuliza kwa nini sisi wenyewe tusiwe na moyo wa namna hiyo, wa kuchangia masuala ya elimu, afya na kadhalika.

Nilifarijika kusikia kuwa mfanyabiashara maarufu Reginald Mengi amechangia shilingi milioni nyingi kuendesha mradi maalum wa OBA, ambao ni shule ya wasichana wa Maasae. Ilikuwa faraja kusikia juhudi za angalau huyu m-Tanzania mmoja.

Uanabodi katika OBA ni shughuli ya kujitolea. Wajibu mojawapo muhimu wa mwanabodi ni kuchangia au kuchangisha hela kwa ajili ya OBA. Napangia kufanya kila niwezalo kutekeleza jukumu hili, pamoja na kuwahamasisha wa-Tanzania wafuate nyayo za Mengi. Hatuna sababu za msingi za kushindwa kuchangia mambo kama elimu na afya, wakati daima tunachanga michango ya sherehe na mambo mengine.

9 comments:

malkiory said...

Hongera sana Profesa Mbele, nadhani hili ni jambo zuri na ni utamaduni mzuri wa kuigwa na watanzania wote bila kujali kipato. Walisema kutoa ni moyo, si utajiri.

Mbele said...

Kuna mambo mengi ya kutisha katika jamii ya Tanzania. Unaweza kupita kwenye kijiji au kamji kadogo, ukakuta shule haina madawati, vitabu, wala vifaa vingine, na watoto wanakaa sakafuni. Halafu hapo hapo kijijini au kwenye kamji unakuta baa zenye viti vizuri, meza nzuri au makochi. Mlevi anaheshimiwa Tanzania kuliko yule anayetafuta elimu.

Halafu, kuna waMarekani wengi huko vijijini wanaojitolea, chini ya mashirika kama Peace Corps Wanajitolea hapo kijijini, kujenga shule, au kuleta vifaa, na wanatembelea baiskeli au basi la kijiji.

Wakati huo huo, vigogo wetu wanakatiza humo vijijini wakiwa na mashangingi ya bei mbaya, halafu wanakuwa wageni rasmi wa kupokea michango ya madawati au maabara kutoka Marekani au Ulaya. Kesho yake tunasoma hayo kwenye vyombo vya habari, bila kujitambua jinsi tunavyojiumbua.

Emmanuel said...

Ninakuombea kila la KHeri Prof katika majukumu hayo mapya.
Tuko pamoja tukiweza kusaidiana pamoja tutaiijenga Tanzania tunayoitaka

Simon Kitururu said...

Pole sana Profesa! Kwa kuwa nahisi shughuli yako ingekuwa ni KICHENI PATI au harusi za kibongo NAHISI ingekuwa rahisi zaidi!:-(

Mbele said...

Ndugu Kitururu, huwa najiuliza itakuwaje nitakaporejea Bongo kimoja. Nahisi nitakuwa daima na majukumu ya uenyekiti wa vikao vya "send-off," arusi na kadhalika, kiasi kwamba sitapata hata muda wa kusoma kitabu :-)

Simon Kitururu said...

@Prof. Mbele: Yani utakoma yani!:-)

Mbele said...

Ndugu Kitururu, si unajua tena, wakishaona una kakofia ka "Prof." au "Dr." basi wewe ni mwenyekiti kila kikao. Yaani unakoma kabisa :-)

Simon Kitururu said...

@ Frof. Mbele: Si umeona Prof. Matondo uliye muambukiza kupasi CHUO KIKUU CHA DAR wakati NGULI anavyodai tusimuite PROF. MATONDO?:-(

Ila kusema ukweli hata wakati mnatukanwa[huwa naona wakataao pointi zako wakutukanavyo!:-(]

mie pointi nazidaka!:-(
Na samahani Prof. kama uhuwa unapitia kwangu kwa kuwa huwa staili yangu ya kuongea huwa haijavalishwa chupi.:-(

Ila na KRITIKI ya vitabuvyako kwa wote walio soma baada ya mimi kusoma ,...
... wewe na NN MHANGO nitamwaga mambo kuhusu vitabu vyenu ila nasubiri watakao kudadavua wamalilize !:-(

Simon Kitururu said...

DUH!!

Ntarudi kudadavua nilichotaka kusema kwa kuwa nilichotaka kusema ni kuna spelingi hovyo kibao ila natumaini Prof. umenielewa!:-(

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...