Sunday, February 20, 2011

Tanzania Yetu ....

Wimbo huu hapa unatukumbusha tulikotoka, na mategemeo yetu miaka ya mwanzo ya Uhuru na hata baada ya "Azimio la Arusha." Tulipata Uhuru tukiwa na matumaini makubwa, na mojawapo alilieleza vizuri Mwalimu Nyerere:

Sisi tunataka kuwasha mwenge, na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, ili umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki, na heshima palipojaa dharau
.

2 comments:

Christian Sikapundwa said...

Profesa Nakushukuru sana kama bado unakumbuka hakima za Baba wa Taifa mwalimu Juius Kambarage Nyerere.

Zile ni zama za kukumbuka kudai uhuru,wewe na mimi ndiyo tuna yajua hayo.Lakini kizazi kipya kina mambo yake Sikakazi ukiwambie waimbe wimbo huo watazima radio ama TV.

Vijana amani kwao si jambo la msingi wanacho dai ni haki ya papo kwa papo ndiyo maana migomo huku kwetu ni fashion.Nakuomba ubarikiwe sana kama bado unajali wapi tulikotoka nasasa tunaenda wapi nchini kwetu Tanzania.Prf.bado tunakazi kubwa kila la kheri.

Mbele said...

Tulipopata Uhuru nilikuwa darasa la tatu. Miaka ilivyokwenda nami kuendelea na shule, watu wa siku zile tulipata fursa ya kusikiliza hotuba za Mwalimu Nyerere na kusoma sana maandishi yake.

Tulioenda Chuo Kikuu (enzi hizo ikiwa ni Mlimani) tuliendelea na mazoea hayo ya kusoma fikra za Mwalimu na wanamapinduzi wengine wengi kutoka sehemu mbali mbali za dunia.

Nami nasikitika ninapoona hali ya vijana wa leo. Sioni dalili yoyote kuwa wako makini katika kutafuta elimu kwa upana wake, na wala sioni dalili yoyote kuwa wamesoma hata haya maandishi ya Mwalimu Nyerere, achilia mbali maandishi ya watu wengine mashuhuri waliouelimisha ulimwengu kuhusu masuala ya mustakabali wa nchi kama zetu.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...