Wednesday, February 2, 2011

Kauli ya Mufti Simba Kuhusu wa-Islam na Elimu

Nimesoma kwa furaha taarifa kuwa Mufti wa Tanzania, Shekhe Mkuu Issa Shaban Simba, amewataka wa-Islam Tanzania wajibidishe na elimu ili kujikomboa kimaisha. Amenukuliwa akisema, "Huu ni muda mwafaka kwa waislam kuanza kujikita na kukazania zaidi suala la elimu, na si kubaki kulialia pekee kuomba kuchaguliwa na kupewa vyeo serikalini, hivyo tuchangamke tusiendelee kubaki nyuma tupige hatua kama wenzetu." Soma taarifa hii hapa.

Nilikuwa njiani kuandika makala kuhusu suala la elimu katika historia ya u-Islam, ili kuiweka katika blogu hii. Baadhi ya mambo niliyopangia kusema ni kwamba u-Islam, tangu mwanzo, ulihimiza suala la elimu katika taaluma mbali mbali. Mtume Muhammad alisisitza suala hilo na waumini wakafuata kwa makini. Anayosema Mufti Simba ndio ukweli kwa mujibu wa dini ya ki-Islam.

Makala yangu inakuja. Kwa leo napenda tu kusema kuwa msisitizo wa Mufti Simba kuhusu elimu unatuhusu sisi wote, si wa-Islam peke yao. Ninaandika sana kuhusu suala hilo kwenye blogu na sehemu zingine, kama vile kitabu cha CHANGAMOTO, nikilalamika kuhusu uvivu uliokithiri miongoni mwa wa-Tanzania katika suala la elimu. Kwa hivi namwunga mkono na kumpongeza Mufti Simba kwa kusimama kidete kuongelea suala hilo. Yeye kama kiongozi wa wa-Islam amewataja wao, lakini ukweli ni kuwa nasaha zake zina manufaa kwa wa-Tanzania wote.

1 comment:

emuthree said...

Elimu ni muhimu kwa kila mwanadamu, ...na ili uijue dunia na mazingira yake inabidi usome. Ni kweli kuna baadhi ya jamii kutokana na sababu fulani zimekuwa zikiwa nyumba kwa elimu, ilihali kama ni `imani' inahimiza kuhusu elimu, je iweje watu hawo wasiendane na imani yao...
Kuna sintofahamu ...kwa vyvyote iwavyo sintofahamu hiyo inajulikana na kama inajulikana basi wakati umefika wa kufuta imani kama inavyohimiza. Ni kwa hali ngumu, lakini hakuna jema bila kuumia..kutafuta kama ilivyosemwa kuwa `tafuteni elimmu hata ikibidi kwenda uchina...' kuna maana kubwa hapo!

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...