Mzee Fultz ni mchungaji wa kanisa la ki-Luteri, sinodi ya St. Paul. Anaishi hapa Minnesota na Iringa, akiendesha programu za ushirikiano.

Tangu wakati kitabu hicho kilipokuwa ni kijimswada tu kisichokamilika, Mchungaji Fultz alikibeba na kukipigia debe hapa Marekani. Hakuwa peke yake katika kufanya hivyo. Nilivyoona hivyo nilishtuka, nikaamua kukifanyia kazi kimswada hiki na kukiboresha.
Kazi hiyo niliifanya kila siku kwa miezi minne, hadi nikakichapisha kitabu mwezi Februari 2005. Mchungaji Fultz alikiandikia makala kwenye kijarida cha kanisa mojawapo hapa Minnesota, mbali na kuendelea kukipigia debe kwenye mikutano mbali mbali na kwa watu binafsi katika maandalizi ya safari za Tanzania. Wa-Marekani wengi wameniambia kuwa walisikia habari za kitabu hiki kutoka kwake. Wengine wamewapelekea nakala wa-Tanzania.
9 comments:
Ni jambo la pekee kabisa unalo lifanya la kumthamini mpiga debe wako.
Kuna baadhi ya watu hajali kama kuna watu wamewasaidia katika mafanikio yao.Wewe Profrsa ni mtu wa watu ndiyo unaenenda kwa mtindo wa maandiko matakatifu.
Shukrani Mzee Sikapundwa kwa ujumbe wako. Nikizingatia kuwa huyu mzee ni mchungaji, juhudi yake inanifanya nitambue kuwa nina wajibu wa kufanya makubwa zaidi, kwa manufaa ya wanadamu. Naamini Mungu ndivyo atakavyo.
Bomba sana yani!
Na inafurahisha kukutana na mtu athaminiye ya mtu kazi !
Shukrani ndugu Kitururu. Nangojea pia siku ya kukutana nawe, maana nawe ni mpiga debe wangu wa kutupwa :-)
@Prof: :-)
Tena itabidi upewe angalau ka-Heineken kamoja na kamguu ka kuku :-)
@Prof: Hiyo si itanifanya ninene kwa lugha kistaili ya wanenao kwa lugha ki kama kimakanisani fulani?
Ila ukweli mie kama ningekuwa tajiri kidoko TU nafikiri uandikayo ningesambaza dunia nzima!
Na mpaka sasa hivi najaribu niwezavyo kusambaza hekima zako kivyangu na nashukuru kama umestukia hilo!
Kwangu wewe ni bonge la SHULE!
Na ujuavyo kurahisisha topiki ngumu zieleweke kirahisi hapo ndipo najua wewe ni mwalimu wa aina gani!
Kwa kuwa naamini dunia ina walimu wengi kwa jina ingawa ukifuatilia unastukia ni walimu jina kwa kuwa hawaweki hata wafundishacho ki mkao watu wawalengaoKUWAFUNDISHA KITU kuelewa wanajaribu kufundisha nini!
Na nashukuru kukustukia mapema na samahani kwa kuwa kama nijifunzayo kwako ungetaka nikulipe nisingeweza Prof. :-(
Huwa napita sana hapa lakini kimya kimya, leo nimeondosha ukimya kwa kuacha alama.
Uishi milele Prof.
Ndugu Mcharia, shukrani kwa ujumbe wako wa mwanzo, nami nakutakia kila la heri. Kuhusu ujumbe wako wa pili, nami nimekuwa nikisoma malumbano kuhusu tuzo kwa wanablogu. Nimekuwa msikilizaji, na papo hapo nakumbuka kuwa nimekuwa nikisema kuwa kublogu kwangu naona ni hasa suala binafsi, kama nilivyosema katika makala hii.
Post a Comment