Tuesday, May 3, 2011

Siku ya Waalimu

Leo, huku Marekani, ni siku ya kuwaenzi waalimu. Wiki hii nzima ni wiki ya kuwakumbuka, lakini leo ni kama kilele. Na mimi, mwalimu wa chuo kikuu, nimeshaandika kuwa namwenzi kwa namna ya pekee mwalimu wa shule ya msingi.



Kwa vile ualimu ni sehemu ya nafsi yangu, huwa natafakari suala la ualimu na dhima yake katika maisha yangu na maisha ya wanafunzi. Leo na wiki hii najisikia furaha kujumuika na wale wote wanaothamini mchango wetu.





(Picha ya kwanza hapo juu niliipata kwenye blogu ya Haki Ngowi, ambaye aliripoti kuwa ilipigwa na Brandy Nelson. Picha ya pili sikumbuki niliipata kutoka blogu gani. Ningependa kutoa shukrani).

3 comments:

Anonymous said...

Kazi ya ualimu ni kazi yenye jukumu kubwa sana.Ni kazi ya kumpa elimu mwanafunzi ambayo ndio maisha yake ya baadae.

Niliwahi kusoma jambo linalihusu ualimu ktk blog moja hivi,lakini ilizungumzia kuhusu shule za "binafsi"na jinsi wanavyo ajiri waalimu kutoka nje ya nchi badala kuwapa ajira walimu wa nyumbani.Na ilikuwa ni mazungumzo makali na kila mtu alitoa maoni vile anavohisi ukweli ulipo.

Ukiangalia shule za serikali utakuta kuna tofauti za walimu ktk mafundisho yao.Wapo walimu walio na hamu ya kufundisha ili mwanafunzi wake aelewe ambao ni sio wengi kwa miaka hii.Na wengine anifanya kazi ya ualimu kutokana hana jinsi nyine ya kazi hivo ni ajira ya kumpatia maisha ya kila siku.Na hapohapo wengine hutoka na kufundisha nje ya wakati wa kazi ili ajipatie senti za nyongeza.

Nimeona tofauti yamimi nilivyosoma nyumbani na hapa uingereza jinsi watoto wangu wanavyo soma shule.Walimu wanajaribu kwa bidii zote kumpa elimu ipasavyo mtoto.Walimu wanasimamiwa ipasavyo ktk ufundishaji wake na kama hajaonyesha mafanikio mazuri kwa watoto kimaendeleo basi na kazi hana.Kila mwaka kama sikosei marambili kunakuwa na uchunguzi maalum kutoka ktk halmashauri zao na kutembelea shule kuangalia "standard" ya shule na elimu anayopewa mwanafunzi.Na vilevile kila mwaka unaweza kuangalia ktk "net"kuhusu shule anayosoma mtoto wako na kujua maendeleo ya shule.Unaweza pia ukajua shule ipi yenye maendeleo mazuri ili kama unataka mtoto akasome shule tofauti.Na vilevile walimu wanajitahidi kadiri ya uwezo wao kuwafundisha watoto na hupenda kuwahusisha wazazi na kuwahamasisha ktk elimu.

Bado kunatatizo kubwa sana kwetu kielimu na hii inatokana na maisha tulio nayo na mengine ni ya kuyaendekeza.Nakumbuka wakati nipo shule mwalimu anakuja na "hangover"ya usiku kuchwa kunywa kupita kiasi.Sidhani kama mtu atakuwa anayo hamu ya kufundisha.Sanana ataingia na kama alisikia mlikuwa mnaongea basi ni fimbo kwenda mbele.Hapo kwanza unakuwa ni muoga kwasababu walimu hawajengi urafiki na watoto ili kujenga "good concentartion"ambayo naamini nimuhimu sana kwa mtoto ili kumjengea shauku la kusoma kwa bidii.

Nadhani ndio maana shule za binafsi wanapenda kuajiri walimu wa nje kutokana na tabia tofauti ili kuweka maendeleo kwa mtoto.Sijui kama utakubaliana na mimi pro..

Mbele said...

Shukrani kwa mchango wako mdau. Nikiongezea hayo uliyotaja, pia wazazi wa kwetu wanapaswa kuamshwa ili wajihusishe na masomo ya watoto wao.

Umetaja huku ughaibuni, nami nafahamu mambo ya Marekani. Huku walimu wanamtegemea mzazi ashiriki kumsaidia mtoto kazi za shuleni. Unajikuta mwanao anakuja na madaftari halafu anakuuliza namna ya kutatua mafumbo katia hesabu, au anakuuliza mambo ya elimu ya viumbe, na kadhalika.

Inakuwa vigumu kumpa mwanao kisingizio kuwa hukusomea masomo hayo. Hatakuelewa. Kwa hivi, unawaibika kujikumbusha.

Kwetu Bongo mambo ni kinyume. Wazazi wengi wakitoka kazini ni mguu kuelekea baa. Huwaoni wanarudi nyumbani na kufuatilia daftari za mtoto.

Kama hawana hela ya bia, basi utawakuta vijiweni humo mtaani, wakilumbana kuhusu Yanga na Simba, au CCM na CHADEMA.

Halafu, tofauti na zamani, ambapo ufundishaji wa shuleni ulitosheleza, leo kuna mkondo wa pembeni pia, yaani "twisheni." Kuwepo na kushamiri kwa "twisheni" ni jambo linalonifadhisha. Lakini hii ni mada ya kuandikiwa makala kamili.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ualimu - Taaluma muhimu kuliko zote lakini inayodharauliwa sana - hasa Afrika.

Sina la kuongezea kwani Anony. na Profesa Mbele mmesema kila kitu.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...