Wednesday, November 16, 2011

Eti Tuupigie Mlima Kilimanjaro Kura, Kwa Lipi?

(Makala hii imechapishwa katika blogu ya kamalaluta)

eti tuupigie mlima kilimanjaro kura, kwa lipi?

sikuupigia kura mlima kilimanjaro na wala sikuwa na mpango wa kuupigia kura na nisingeweza kuupigia kura. ni kweli ungekuwa maajabu ya dunia tungepata pesa nyingi. lakini kwa nini kushiriki kuupigia kura mlima kilimanjaro??

Tanzania hupata pesa nyingi kutokana na utalii, ufadhili na vyanzo vingine.lakini pesa hizo huishia wapi?? tunazidi kukamuliwa kodi na kumasikinishwa. wakulima kama mimi tumekosa mitaji, huku rais wetu akionekana kila siku anawakaribisa matajiri kutoka nje ili wajekuchukua vijishamba vyetu kuwekeza eti.

mapato yoote hayo pamoja na utalii huishia wapi? hamna huduma za msingi za jamii, shule alizozijenga nyerere ndo bado zipo zinakaribia kuwaangukia wanafunzi.

pesa za kufisidi huwa hazikosi na mafisadi wako huru kuiba watakacho, anasa za watawala nazo hazikosagi pesa. wananunua magariya kitajiri, pinda eti anakataa gari la kitajiri kwa kuwa anaendesha gari la kitajiri then gari alilolikataa linapelekwa kwenye idara nyingine, kwa nini kuupigia kura mlima huu?

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni swali nzuri sana kwa lipi???

Anonymous said...

kwa kweli ni swali zuri sana, 'kwa lipi?' lakini, kwani ukiacha kupiga kura ndo pesa zitaacha kuliwa?cha msingi ni kupambana noa mpaka kieleweke,vp kama siku za mbeleni akipatikana serikali inayojali mambo uliyoyataja hapa, hauoni kwamba utajilaumu kwa kutokuupigia kura mlima kilimanjaro na kupunguza mapato kwa serikali inayojali? roma haikujengwa kwa siku moja, piga kura kwanza, halafu mambo mengine baadae, ITAFAHAMIKA TU.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...