
Leo nilikwenda Apple Valley, kuongea na wanafunzi wa
Chuo cha Msomo ya Mazingira. Nilialikwa na mwalimu Todd Carlson, na wanafunzi wake hao wamekuwa wakishughulika na mada ya falsafa za jadi.
Kwa miaka mingi, mwalimu Carlson amekuwa
akinialika kuongea na wanafunzi hao.

Katika kuwaandaa, Mwalimu Carlson anawapa sehemu kadhaa za kitabu cha
Matengo Folktales wasome. Kutokana na maandalizi hayo, wanafunzi hao wanakuwa na duku duku na masuali mengi ya kuniuliza. Ni wanafunzi makini sana. Wanaulizia kuhusu utafiti wa fasihi simulizi na changamoto za uandishi masimulizi hayo, tafsiri, maana, falsafa na kadhalika, wakizingatia yale niliyoandika katika
Matengo Folktales.
Kila ninapotembelea
Chuo hiki, nawasimulia hadithi angalau moja kutoka katika
Matengo Folktales. Leo niliwasimulia hadithi ya "Jitu Katika Shamba la Mpunga," ambayo ni chemsha bongo ya aina yake, tukatumia muda kuiongelea.
No comments:
Post a Comment