Saturday, April 20, 2013

Binti Zangu Wamewajibika Leo Minneapolis

Leo binti zangu wawili wameshiriki mbio za kuchangia taasisi ya mafunzo iitwayo ThreSixty Journalism. Mbio hizi zimefanyika asuhubi leo mjini Minneapolis.

Mwaka 2009, binti huyu mwenye kitambaa kichwani alichaguliwa kusoma katika taasisi hiyo. Huchaguliwa vijana kadhaa kutoka shule mbali mbali. Wakiwa kwenye taasisi hiyo husomea masuala ya uandishi katika magazeti na vyombo vya habari kwa ujumla. Ni fursa inayothaminiwa sana. Vijana hupata mafunzo bora kitaaluma, na pia fursa ya kukutana na waandishi na wanahabari maarufu. Kama sehemu ya mazoezi, binti yangu alipelekwa kwenye jamii ya wa-Somali hapa Minneapolis kufanya nao mahojiano, akachapisha makala hii hapa. Makala yake hiyo, na nyingine, zilichapishwa pia katika Twin Cities Daily Planet na Star Tribune, ambayo ni magazeti maarufu hapa Minnesota.

Nimefurahi binti zangu wamechukua uamuzi kulipia ushiriki wa mbio hizo, kuchangia taasisi hiyo. Napenda waendelee katika moyo huo.

2 comments:

Rachel siwa Isaac said...

Hongereni sana mabinti...@Zawadi kazi nzuri sana MUNGU azidi kukusimamia..

Pia ni mfano mzuri kwa Wadogo zako/watoto wetu wengine..

Asante PROF MBELE.

Mbele said...

Asante, Dada Rachel, kwa ujumbe wako, na nasaha. Ni kweli, nikitafsiri wazo lako, kulea watoto ni kwa kusaidiana na kushirikiana. Asante sana nawe.