Friday, June 27, 2014

Ninaendelea Kupona

Picha hizi nimejipiga mwenyewe dakika chache zilizopita, mchana huu. Ninajaribu kujizoeza mtindo huu wa kujipiga picha. Lakini vile vile, nimeona niziweke hapa, ili kuwathibitishia ndugu, marafiki na wengine wanaonikumbuka, kwamba hali ya afya yangu inaendelea kuimarika. Wasiwe na wasiwasi sana juu yangu. Yaonekana Mungu ameamua niendelee kuwepo duniani na kutekeleza majukumu kwa jamii.

Nawashukuru wote kwa kuniombea, nami, kama nilivyowahi kutamka, nategemea kuingia tena darasani kufundisha wiki ya kwanza ya Septemba, utakapoanza muhula mpya.

Hiki kikofia nilichovaa alininunulia binti yangu Zawadi. Ninakipenda sana, hasa kwa vile tuko katika kipindi cha jua hapa Marekani.

2 comments:

Theo said...

Pole sana Profesa.Mungu akujalie afya njema na nguvu uweze kuendelea na kazi yako ya kuelimisha.

Mbele said...

Shukrani kwa ujumbe. Nawe Nakutakia afya njema na kila la heri.