Thursday, June 12, 2014

Tuyatunze Mazingira

Kitu kimoja kinachofurahisha hapa ninapoishi na kufanya kazi, ni jinsi mazingira yanavyotunzwa.
Kila siku naenda nje na kunyoosha miguu, ili kusaidia uponaji wangu.
Nina mazoea ya kuketi na kuangalia mimes mbali mbali, maua, na nyasi zilivyokatwa vizuri au zilivyoondoshwa ili kuipisha miti ya maua.. Ni mazingira yanayopendeza sana.Ndege wa aina aina wanafuata sehemu hizo, nami nimezoea kuwaangalia. Wanapendeza.


Vinyama vidogo vidogo naviona vikicheza.

Hewa ni safi. Inaburudisha nafsi. Mazingira yamependezeshwa pia kwa maua.


Hapa nimeweka picha kadhaa nilizopiga hatua chache kutoka maskani yangu.

Hakuna takataka kama vile plastiki, matairi yaliyochakaa, makopo, na uchafu mwingine ambao umesagaa sehemu nyingi za nchi kama Tanzania.

Baada ya kuyazoea mazingira haya safi, nakerwa  kuangalia hali kama ile ya Dar es Salaam. Inakuwa vigumu kuamini kama mji ule wanaishi watu.

Milima ya takataka imezagaa mitaani.  Mitaro yenye maji machafu sana inapita humo mitaani. Hakuna anayeshtuka kuona ukatili huu wa kutisha dhidi ya mazingira. Waliosoma na wasiosoma na hao tunaowajta viongozi, wote hawana elimu. Wanaendeleza ukatili huu dhidi ya mazingira, pamoja na kwamba hali hiyo ni chimbuko la magonjwa.

2 comments:

PBF Rungwe Pilot Project said...


Umegusia suala nyeti sana Profesa. Mimi nadhani ni wakati mwafaka suala la mazingira likaingizwa hata kwenye mitaala ya shule za misingi na sekondari ili kujenga jamii anayoelewa umuhimu wa mazingira katika maisha ya mwanadamu.Aidha, kutoa fursa za wanafunzi kusafiri maeneo/ nchi za wenzetu kuona wanavyotunza mazingira na hatimaye kupata hamasa ya kufanya hivyo.

Anonymous said...

Kuna Kitu Mie ni kijana wa miaka 30 kuna siku niliona kwenye TV, watu wanalalamikiana chuo kikuu Mlimani vyoo vinaziba, Mie nikawaambia tatizo sio watumiaji tatizo Chuo Kikuu chenyewe na TV zetu wasomi wengi wanatoka maeneo hawajui kutumia vile vyoo sio Kama utawazarau ila chuo kina makosa wanatakiwa kuwapa Elimu ya kutumia vyoo Hivyo na pia Elimu kwenye ma TV ya kusafisha na kutumia vyoo vya aina tofauti Kama Uwanja wa Taifa ulivyofunguliwa watu walikojoa kwenye ma sinki, TV kazi kuonyesha ujinga, muhimu community zingekuwepo mtaani kila nyumba 10 zinatowa watu wake kusafisha mtaani mwao kushindana na mitaa mengine tungekuwa mbali na Maradhi ila wajumbe wa nyumba 10 Kumi kazi Yao kusikiliza kesi za mke na Mume au wapangaji basi.