Saturday, January 24, 2009

Chakula Bora

Niliwahi kuandika makala, Kuku kwa Mrija. Leo nimeona nilete makala juu ya vyakula anavyokula Rais Mpya wa Marekani, Barack Obama, makala ambayo inasisitiza umuhimu wa kuangalia tunakula nini, na inaonyesha kuwa kiongozi anaweza kutoa mfano kwa wananchi. Kama nilivyosema katika ile makala ya Kuku kwa Mrija, kuna tabia mbaya inayojengeka miongoni mwa Watanzania, ya kushabikia vyakula ambavyo au havina faida kiafya au vina madhara kiafya. Lakini kutokana na kasumba, watu wanaona wanajipatia hadhi ya juu kwa kutumia vyakula hivi.

Makala ninayoleta hapa imeandikwa kwa kiIngereza, na ingawa blogu yangu hii inatumia kiSwahili, nimeona nivunje utaratibu huu kutokana na umuhimu wa suala la chakula. Ninategemea kuwa wale ambao hawajui kiIngereza labda wataweza kupata msaada wa kutafsiriwa makala hii. Watanzania na wengine wote tunaweza kujifunza mengi kutokana na makala hii inayomhusu Rais Obama. Soma hapa.

2 comments:

Bennet said...

Samahani nimikosa e mail yako kwa hiyo nikashindwa kukutumia mail ya peke yako naomba usome link hizi zifuatazo kisha unawezakufuta maoni yan gu na kutuandalia makala ili tupate maoni tofauti

http://www.wcs.org/353624/kihansispraytoads

http://news.mongabay.com/2005/0606-Kihansi_Spray_Toad.html

Mbele said...

Hapana tatizo. Anwani yangu ni info@africonexion.com.

Nimesoma hizi taarifa ya vyura. Sina hakika kama nina ujuzi wa kutosha katika suala hili. Itabidi niendelee kujielimisha.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...