Friday, January 9, 2009

Mfano Bora wa Ujasiriamali

Neno ujasiriamali linasikika sana miongoni mwa Watanzania. Wengi wanajitahidi kuanzisha shughuli mbali mbali za kutoa huduma, kuuza bidhaa, na kadhalika, kama njia ya kujiongezea kipato na kujiendeleza kimaisha.

Lakini, wengi hawana ufahamu wa siri ya mafanikio na maendeleo katika shughuli hizo. Kutokana na hilo, wengi wanashikilia imani za ushirikina. Matokeo yake katika jamii yetu yamekuwa mabaya sana, kama vile mauaji ya watu wengi. Hali hii inatisha. Kwamba watu wanaamini kuwa vitendo hivi vya kishirikina ndivyo vinaleta mafanikio ni ishara ya kukosekana elimu katika jamii yetu, ikiwemo elimu ya kuendesha miradi mbali mbali.

Napenda kuleta taarifa kuhusu mjasiriamali mmoja ninayemfahamu, ambaye naamini anaonyesha mfano wa kuigwa na wajasiriamali wa Tanzania. Anaendesha mgahawa uitwao Tam Tam, katika mji wa Minneapolis, Minnesota. Ni mtu anayejibidiisha kufahamu biashara yake, wateja, na mambo mengine kadha wa kadha. Anajua kuwa elimu ni ufunguo wa mafanikio. Taarifa hizi zimeandikwa kiIngereza, lakini wengi wataweza kuzisoma na labda kuwaeleza wasojua kiIngereza. Soma hapa na pia hapa.

2 comments:

Unknown said...

Naitwa Charles Nazi
Asante sana kwa kuelimisha jamii mimi niko huku Tanzania ninaendelea kutoa mafunzo ya ujasiriamali tembelea squidoo yangu
http://www.squidoo.com/mshauricharles

Mbele said...

Shukrani kwa ujumbe wako. Nimeangalia squidoo yako yote. Unafanya kazi nzuri. Nimepita pia kule lulu.com nikaona vitabu vyako. Ni jambo zuri kuwa nawe unahimiza elimu. Kila la heri.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...