Wednesday, October 6, 2010

Chukua Chako Mapema

Pale CCM ilipoanzishwa, baadhi ya wa-Tanzania walianzisha minong'ono wakitafsiri CCM kama "Chukua Chako Mapema."

Nilitaja jambo hilo katika makala fupi, "Jokes Play Social Role," ambayo ilichapishwa katika gazeti la Daily News (Tanzania) (Juni 16, 1987) ukurasa 4.

Ni miaka mingi imepita, na ushahidi wa nini hasa maana ya CCM umeendelea kujitokeza. Tumsikilize katibu mkuu wa CCM:

7 comments:

Simon Kitururu said...

DUH! Nahamu ya kusikia hotuba nzima maana kirahisi nisije tafsiri vibaya anamaanisha nini!

Mbele said...

Ni kweli. Ingekuwa hao jamaa hawakwepi midahalo, tungeweza kuwauliza watueleze kinaganaga.

malkiory said...

Kituru hapa bila hata kuangalia hotuba nzima. Umasikini wa watanzania kwa miaka 49 ya uhuru ni kielelezo tosha kuwa CCM maana yake ni "Chukua Chako Mapema"

Subi Nukta said...

Wakuu, video hizi zipo katika tovuti ya Phillip Mogendi, ukifungua tovuti hiyo, tizama kulia bofya kifute cha Documentary, utaziona kwa ukamilivu sehemu 1 - 3. Pia zipo wavuti.com hapa sehemu ya "videos"

Mbele said...

Dada Subi, shukrani kwa kutuelekeza kwenye video hizo kwenye tovuti ya Philip Mogendi. Nimeona ile ya tatu, jinsi wananchi wa Tarime wanavyolalamika kuhusu matusi waliyotukanwa na viongozi wa ngazi ya Taifa wa CCM, akiwemo katibu mkuu wa CCM.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

CCM kwa sasa ni:
Chukua Chako Mapema
Chukua Chao Mapema
Chakachua Chezea Maadili
Chama Cha Mafisi
Chama Cha Mafisadi,
Chama Cha Ma-ulaji
Chama Cha Maswahiba,
Chama Cha Makupe (Magabacholi kama Jeetu, Somaiya, Chande, Dewji, Abood na wengine)
Chama Cha Mauzauza, (rejea kina Kinana na mahabithi Makamba, Salma, Ridhiwan, JK na wengine wanavyohangaika kujitoa mnasoni)
Chama Cha Maruhani (Wapiga kura hewa na wakuu wa tume mfu ya uchafuzi NEC)
Chama Cha Mabeberu (Kinaendeshwa kwa tamaa na jinai ya kina Rostam, Lowassa, Karamagi, Mramba na majambazi wengine waitwao waheshimiwa)
Chama Cha Maangamizi (Angalia wabongo wanavyozidi kuangamia wakiambiwa wanapelekwa Kanani wakati wanaswagwa kuelekea motoni),
Chama Cha Mufilis (Miradi maarufu ni EPA, Richmond, CIS, Meremeta, SUKITA, mvua za Lowassa na ujambazi mwingine)
Chama Cha Mazingaombwe (Sanaa)
Chama Cha Mizengwe (Kuenguana na kulindana)
Chama Cha Maanguko (Kinapumua kwa msaada wa Redet, Synovate, Luis Makame, Lt Gen Shimbo, Majini ya tapeli shehe Yahya na upuuzi mwingine)
Chama Cha Matapeli (Waandishi uchwara wanaomraba JK mata.... sorry mananihino)
Chama cha..... malizia ad infinitum

Christian Bwaya said...

Hawa wenye hiki chama wanadhani kitabaki madarakani milele! Subiri wiki ijayo tuone kama wataendelea kusema sema kama huyu!

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...