Monday, October 4, 2010

Mahojiano Yangu "Kombolela Show"

Tarehe 2 Oktoba, nilihojiwa katika "Kombolela Show." Hiki ni kipindi cha redio kinachoendeshwa na Jaduong Metty, ambaye pia ni mmiliki wa blog ya Metty's Reflections. Kusikiliza mahojiano, bofya hapa au hapa

4 comments:

malkiory said...

Profesa, Mbele. Mahojiano ni mazuri lakini nadhani recording haikuwa nzuri. Sijui kama ni speaker za pc yangu ndizo zenye kukoroma. Lakini nahisi ni audio recorder haikuwa katika kiwango cha juu.

Mbele said...

Shukrani kwa ujumbe. Nimeongea na wahusika, na wanasema nao walitambua tatizo hili na wako njiani kulirekebisha. Mategemeo ni kuwa sauti itasikika vizuri wakishafanya haya marekebisho.

Yasinta Ngonyani said...

Nimeyasikiliza mahojiano na nimeyapenda sana. Ni kweli kulikuwa kama sauti zilikuwa zinaingiliana vile. Ila ni mahojiano mazuri sana ningefurahi kama wengi wangesikiliza. Binafsi pia nilikuwa na swali hili hivi kwa nini waTanzania huwa tunashindwa kujieleza pale tunapotakiwa kujieleza?

Ni hayo tu kwa sasa

Mbele said...

Dada Yasinta, shukrani kwa ujumbe wako. Nimevutiwa na suali lako kuhusu suala la wa-Tanzania kujieleza.

Labda huwa hatujui mada husika, hasa kwa vile hatuna utamaduni wa kujisomea na kujielimisha kwa ujumla, au hatujiamini, na ndio maana tunatoroka midahalo :-)

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...