Monday, May 2, 2011

Watu Wema Wasio na Dini

Katika mizunguko yangu hapa duniani, nimepata kukutana na watu wasio na dini, lakini ni watu wema sana, waungwana. Sio wachokozi au watu wa majungu. Ni waaminifu, wala hawatakudhulumu. Nimefanikiwa kufahamiana na kuishi na watu wa aina hiyo. Wengine wamekuwa wanafunzi wangu huku ughaibuni.

Ukiwauliza kuhusu dini, wanakuambia hawaamini kama kuna Mungu, na hawana dini. Hao watu ni changamoto kubwa kwetu sisi tunaosema tuna dini, hasa pale inapokuwa kwamba hatuwafikii kwa wema na utu. Ni kitendawili. Inakuwaje watu hao wawe hivyo walivyo, wakati hawana dini? Kazi kwenu wadau.

6 comments:

Anonymous said...

Unajuwa pro..sukuzote mimi nilivyo na tabia yangu huwa sipendi kumjaji mtu kwa dini.Itakuwa sio halali kama ilivo kumdhania mtu bila ya uhakika wa kuona na kuhakikisha mwenyewe kwa macho.Kwasababu dini ni imani ya mtu kuamini kuwepo kwa mungu au kutokuamini kuwepo kwa mungu.Kwa upande wangu ni jambo zuri sana kumuamini mungu lakini binaadamu hutofautiana na vilevile wanakuwa na sababu zao za kukataa kuwepo kwa mmungu.Ukija kitabia hilo ni suala tofauti kabisa japokuwa inakuwa na muelekeo mzuri ktk imani ya dini.Tabia kwa mimi naamini malezi kutoka kwa wazazi inachangia mambo mengi sana.Kwasababu ktk familia ya watu wenye kuamini mungu kunaweza kukawa na dosari ya kulea watoto na watoto wakaondokea kuwa ni watoto watukutu na hawana heshima na kudharau watu.Ama wanaweza kuwa na tabia ya kudhuru watu na heshima zao au kudharau dini za wenzao.Hivyo tunapaswa kuheshimiana kama binaadamu wakawaida bila kujali dini au rangi ya mtu.Hakuna aliyezaliwa kwa kukamilika lazima tunatofautiana kitabia na tabia ni jambo zito sana kwasababu linabeba maisha ya mwanadamu.Kwa hiyo pro.. tusiwajaji watu kwa dini tuwajaji kwa tabia nadhani ndio tutapata jibu la ukweli.

Yasinta Ngonyani said...

Hakika hiki ni kitendawili haswa,... Kuamini kama kuna mungu au sio na kumuhukumu mtu bila kumfahamu...nakuna kichwa kwanza..

emu-three said...

Kweli watu kama hawo wapo, ...dini ipo, lakini kama mtu mwenyewe huna `uwema' hata ukijifanya una dini na mateno yako yakwa kinyume na yale maandiko ina maana gani!

Anonymous said...

Prof:

Hata mimi katika kuzungumzia tofauti za dini hupenda kutumia hawa watu kama mifano katika kupambanua ipi yaweza kuwa dini ya kweli (kwa leo tuu). Maana kwa mujibu wa Korani: Uyahudi, Ukristo, na Uislamu ni dini moja yenye majina tofauti kwa nyakati tofauti, kwani Mungu ni mmoja hawezi kuleta dini tofauti tena zenye misingi tofauti.

Kwa mujibu wa Korani, Uyahudi ni dini ya kweli kabla tu ya kuja kwa Yesu, na ukristo ni dini ya kweli kwa wakati kabla ya Muhammad tuu. Kwa maana nyengine ukweli wa dini hutegemea wakati.

Naamini dini ya kweli ni ile tuliyonayo kwenye asili ya maisha yetu, kabla ya kunongonezwa na mzungu, mwarabu, au babu jongo (wa matambiko).

Tunavyovaa, tunavyojali watu wengine, tunavyokula, tunavyolinda jamii, n.k.

Nilimwuliza mlokole mmoja,"mbona wapagani hawasali kabla ya kula lakini Mungu huwapa afya katika chakula hicho?" Hakunijibu.

Nikamwmbia kusalia chakula si chanzo cha nguvu na baraka katika chakula bali uhalali wa riziki ile ndo baraka.

Mbele said...

Wadau hapa juu, shukrani kwa maoni yenu. Katika historia watu wengi wanaosema ni waumini wa dini wameleta maafa makubwa, uhasama na vita, kwa kisingizio kwamba wanatetea dini. Kumekuwa na ukatili wa kutisha, na damu imemwagika sana kwa namna hiyo.

Elias Ibrahim Mhegera said...

nadhani pamoja na dini utu wa mtu pia huchangiwa na mazingira alimolelewa namaanisha familia yake, wazazi na watu wanaomzunguka hao ndiyo humuumba mtu atakayekuja kuishi kwa upendo au kwa ubaya katika jamii

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...