Sunday, June 12, 2011

Anonymous Anasema Kitabu Hiki Hakina Jipya

Kwa wasomaji wa blogu yangu hii na ile ya ki-Ingereza, habari za kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences sio ngeni. Wengi wamekisoma kitabu hiki na wengine wamechangia maoni yao katika blogu hizi na zingine.

Juzi ametokea anonymous kwenye blogu hii akaandika hivi: "Nimekisoma hakina chochote kipya, ni kama vitabu vingine."

Mimi kama mtafiti na mwalimu huhamasisha elimu na kuelimishana. Nilimpa ukumbi anonymous atuelimishe zaidi na pia kututajia hivyo vitabu vingine. Habari kamili iko kwenye sehemu ya maoni hapa. Hadi sasa anonymous hajasema kitu tena. Bado nasubiri.

7 comments:

Simon Kitururu said...

Anony eeeh! Njoo basi ufungue ukurasa mpya katika swalaili shule ipanuke kama kweli wewe una jipya!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kupingwa, na hata kukandiwa ni jambo la kawaida - katika taaluma na kwingineko. Hata uandike kitabu kizuri namna gani lazima tu utakuwa na wapinzani. Biblia yenyewe mpaka leo bado inaandamwa.

Hata wapinzani wa Albert Einstein mpaka leo bado wanajaribu kuhakiki baadhi ya nadharia zake - na wengine wanakubali kwa shingo upande pale inapobainika kwamba alikuwa sahihi.

Kupingwa na kukandiwa nadhani ni jambo zuri kama linafanywa katika mjadala unaozingatia hoja kwani kwa kufanya hivyo ndivyo mawazo mapya huenguliwa na mawazo kuu kuu kuimarishwa zaidi.

Kama huyu anony yuko siriazi bila shaka atarudi na kutoa hoja zake. Pengine hoja zake unaweza kuzizingatia utakapokuwa unaandaa toleo jipya la kitabu hiki.

Anony - leta hoja zako!

bibi Alesha said...

Kaka Mbele, huyo alosema hajui asemalo sababu, mimi baada ya wewe kunitumia hicho kitabu, nilikisoma halafu watu wa hapa Marekani walianza kukiazima kwangu na mpaka leo sijakiweka kwenye macho. Kila mtu anakisifia hasa watu ambao hawajawahi kufika Africa wanastaajabu jinsi tunavyoweza kustahimiliana kitu ambacho wengi wa watu ambao hawajatembea kinawashinda.

Tumsubiri huyo atoe mawazo yake.

tz biashara said...

Prof...We kaza buti wala usiwasikilize watu wasiopenda hicho kitabu.Kama hajapenda basi atunge chakwake na akilete uwanjani.

Katu said...

Hongera Profesa Mbele kwa kufungulia mwanga wa kutambua changamoto zinazotukabli duniani hasa kwenye tamaduni zetu...

Ulichofanya wewe Profesa Mbele kwa kitabu ichi ni kuweka kwenye maandishi vitu muhimu hiyo ni sawa na Marehemu Mzee Lauwo alipokubali kupanda mlima kilimanjaro hadi kileleni kwa Mara kwanza kumsindikiza Dr Livingstone wakati huo Mzee Lauwo akionekana kama msaliti kwa imani za kichaga kwamba amevunja mwiko kwa kwenda eneo Mungu wao...

Leo hii kitendo alichofanya Mzee kimeleta neema kiuchumi kwenye nyanja ya utalii...Hivyo anonymous ni sawa wale waliopinga marehemu Mzee Lauwo Mungu amlaze pema peponi...

Hivi sasa hata mimi hicho kitabu kimenifungua kweli uelewa wangu kuhusiana na changamoto zinazokabila jamii nyingi duniani.

Kimsingi huyo anonymous ameshindwa kuelewa kitabu hicho kilichoandikwa...Labda Ushauri hiyo lugha iliyotumika hapo ni kikwazo...

Ombi kwa Profesa Mbele toa toleo liloliyotafsiriwa kwa kiswahili labda inaweza kumsaidia anonymous!!!

Kumwelewesha huyu anonymous kama unavojua tena sisi angalau kiswahili tunawwza kubahatisha kuelewa..

Profesa Mbele kaza buti tupo pamoja nawe...huyo anonymoous ni sawa na mawimbi uchwara baharini......

Mbele said...

Nimempa anonymous uwanja amwage sera, wala sikumwekea kizuizi chochote. Huenda ameingia mitini na hatapatikana tena :-)

Au labda amejichimbia jikoni anakaanga hoja za kukisambaratisha kitabu, na pia kuwasambaratisha akina Kitururu ambao walikipigia debe kwenye blogu zao :-)

Kama anonymous yuko katika hayo maandalizi, basi tukae mkao wa kula :-)

Mbele said...

Kwa mwaka mzima na miezi kadhaa nimemsubiri anonymous atuletee majina ya hivyo vitabu alivyodai vipo, na hadi leo hajafanya hivyo.

Kama ilivyo kawaida katika hizi blogu, wadau wana uhuru wa kutembelea mada zilizopita, na nimeona wako wanaosoma mada hii. Kwa hivyo, nimeona ni vema nikasema kuwa nahisi anonymous huyu ni mbabaishaji anayejifanya anajua.

Wako maprofesa wengi hapa Marekani wanaokitumia kitabu hiki, lakini napenda tu nilete ushuhuda wa hivi karibuni wa maprofesa wawili ambao wamekuwa wakikitumia kwenye programu ya kupeleka wanafunzi Tanzania. Soma hapa.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...