Friday, August 10, 2012

Maprofesa Wanakipenda Kitabu Hiki

Siku chache zilizopita, nimeona makala ya Elizabeth M. Cannon na Carmen Heider ambao ni maprofesa wa Chuo Kikuu cha Wisconsin-Oshkosh. Wameelezea jinsi kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences kilivyowasaidia katika ufundishaji wa wanafunzi waliowaleta Tanzania kimasomo. Makala yenyewe ni "A Study Abroad Program in Tanzania: The Evolution of Social Justice Action Work," Humboldt Journal of Social Relations, 34 (2012), 61-84

Maprofesa hao waliwaleta wanafunzi Tanzania mwaka 2008, 2010 na 2012. Pamoja na mambo mengine, wameelezea matatizo waliyoyapata katika kuwahamasisha wanafunzi kwenye vipengele kadhaa vya masomo yao. Hatimaye walitafuta njia ya kukitumia kitabu cha Africans and Americans katika mijadala darasani, kwa kuwapangia wanafunzi sehemu za kusoma ili waongoze majadiliano darasani. Mkakati huu ulileta mafanikio mazuri, kama wanavyoeleza hapa:

We also thought carefully about how to design our on-site class sessions to reflect our commitment to active, student-centered learning and provide general guidance to our students. We decided to focus these classes on Mbele's Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, on of our readings from 2008, because this Tanzanian author challenges stereotypes through the presentation of his cultural experiences. Before we left the United States, we divided students into four groups and assigned each a section of this text on which they would lead one of four on-site class sessions. On-site discussions focused on comparisons between Mbele's views on Tanzanian life and students' interactions with the people they met and the places they visited. Frustration was replaced with excited conversations. These classes shifted from tense obligations where learning was stifled to an exciting component of the trip where insights flourished. (uk. 68)

Sina la kuongeza. Namshukuru Mungu kwa kunijalia fursa na uwezo wa kukiandika kitabu hiki kwa namna nilivyokiandika, hadi kimekuwa msaada kwa walimu, wanafunzi, na jamii kwa ujumla. Mungu bado ameniweka hai. Wajibu wangu ni kuendelea kujielimisha kwa bidii na kuandika.

4 comments:

anjela said...

big up profesa,mimi nitakipataje kwa hapa belgium?

DAUD said...

nabii hakubaliki nyumbani,hongera sana kwa kukubalika na jopo la wasomi,maprofesa wa nje na kukiamini kitabu chako cha AFRICAN AND AMERICAN EMBRACING CULTURE DIFFERENCES which is a must read book if we are to enjoy cultural diversity in the globe.ilhali nyumbani tukiwa hatuna hata lepe la shukrani juu ya uwakilishi wako kwetu huko ughaibuni katika tasnia ya uandishi na masuala ya linguistics and folktales.hongera mwl mbele kwa uhodari na ushupavu wako.

Mbele said...

Ndugu Anjela, shukrani kwa ujumbe. Kitabu hiki kinapatikana mtandaoni, hapa.

Kama unavyoona, kinapatikana kama kitabu cha kawaida, na pia kama kitabu pepe ("ebook").

Vile vile, unaweza kukiagiza kwenye maduka mengine ya mtandaoni, kama vile Amazon.com.

Kinapatikana pia Dar es Salaam, simu namba 0754 888 647 au 0717 413 073.

Ninaweza pia kukuletea nakala.

Mbele said...

Ndugu Daud, asante kwa nasaha zako. Bahati nzuri ni kuwa mimi napenda sana kufanya shughuli ninazofanya. Ninajituma sana katika kujielimisha na kuwamegea wengine kile ninachokijua, kwa njia ya mazungumzo, mihadhara, na uandishi.

Sibagui. Maandishi yangu yako hadharani, na yeyote anaweza kuyapata. Kuhusu wa-Tanzania, naona wamegawanyika. Vyuoni wanathamini sana kazi zangu. Nafahamu hivyo kwani navitembelea vyuo mbali mbali kila ninapokuwa Tanzania.

Katika jamii kwa ujumla, kuna tatizo la watu kutojishughulisha na vitabu vya aina hii ninavyoandika. Lakini hapa Marekani, jamii imeamka tangu zamani. Leo hii, kwa mfano, ninaenda kwenye maonesho kwenye mji wa Brooklyn Park, Minnesota, na nitakuwa na meza ya vitabu vyangu na machapisho mengine. Kila ninapofanya hivyo, watu wengi wanakuja kwenye meza yangu kuongea nami, kuangalia vitabu, na kuvinunua.

Tanzania nimeshiriki maonesho kama haya mara kadhaa. Watu wazima ni nadra sana kuhudhuria. Utawakuta zaidi watoto wa shule.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...