Kama kawaida, wauza bidhaa mbali mbali walikuwepo. Hili banda lilikuwa na kaseti za hotuba za wanamapinduzi mbali mbali waliojihusisha na harakati za wa-Marekani Weusi. Kulikuwa pia na t-shirts na vitu vingine, vyenye picha za watu maarufu kama Marcus Garvey, Bob Marley, na Malcolm X. Hapa nilinunua t-shirt yenye picha ya Bob Marley.
Hao jamaa, wenye asili ya Jamaica, walikuwa wanauza chakula.
Tamasha la Afrifest ni fursa ya wafanya biashara kuleta bidhaa au huduma zao. Hapa kushoto kabisa ni banda la benki ya Wells Fargo. Tamasha kama hili kwa vile ni fursa ya kuwapata wateja wapya.
Hapa ni wachezaji wa soka wakiingia.
Shughuli za Afrifest ni kwa ajili ya watu wa kila rika. Watoto nao hushiriki.
Hapo ni uwanjani, timu za soka zilipokuwa zinachuana.
Hapa naonekana na mdau.
Hao jamaa ndio walikuwa wanaburudisha umati kwa muziki, siku nzima. Wako hapa na mitambo yao.
2 comments:
prof asante kwa Kutuwakilisha
Shukrani. Najitahidi kuhudhuria shughuli hizi bila kukosa. Zikitokea wakati niko Tanzania, binti yangu anaenda kuniwakilisha. Tangu alipokuwa mdogo, alipenda kutanguzana nami katika shughuli hizo, na tayari aliweza kuongelea shughuli zangu wakati akihojiwa na vyombo vya habari.
Kwa watoto tunaowalea huku ughaibuni, shughuli hizi ni njia moja nzuri ya kuwafundisha kuhusu nchi zetu za Afrika na tamaduni zake. Ni njia ya kuwakutanisha na watoto na watu wengine wa nchi mbali mbali.
Kinachosikitisha, upande huu nilipo, ni kuwa wa-Tanzania hawashiriki shughuli hizo. Wa-Afrika wa nchi zingine utawaona, lakini si wa-Tanzania. Mwaka juzi, kwa mfano, nchi nyingi za Afrika zilikuja, wakaweka bendera zao kwenye meza zao. Hapakuwa na meza ya Tanzania. Mimi nilikuwa nimejiendea pale kama m-Tanzania binafsi, wala sikujua kuwa wenzetu wamekuja na bendera za nchi yao.
Hii ndio hali halisi ya wa-Tanzania upande huu ninaoishi. Tuko wengi, lakini kwenye shughuli za aina hii, humwoni mtu. Nimehudhuria "Twin Cities Book Festival" mwaka hadi mwaka. Na hapo kuna waandishi, wachapishaji wa vitabu, wahariri, wauza vitabu, na wengine wengi. Lakini m-Mtanzania humwoni hapo. Habari ndio hiyo.
Post a Comment