Sensa ni muhimu kwa nchi yoyote kwa maana kwamba ni sherti serikali ijue idadi ya watu wake na mahali wanapoishi.
Takwimu na taarifa hizo ndio msingi wa upangaji wa mipango yoyote ya huduma na maendeleo. Kwa akili yangu finyu, huu ni ukweli usiopingika.
Kama kuna sehemu ambapo watu hawajahesabiwa, sehemu hiyo itaonekana iko wazi; haina watu. Kwa maana hiyo, hakutakuwa na msingi wowote wa kuiingiza sehemu hiyo katika mpango wa huduma au maendeleo.
Sehemu itakayoonekana haina watu itawekwa kando katika mipango hiyo ya huduma na maendeleo. Sasa basi, endapo kulikuwa na watu sehemu hiyo, ambao walisusia sensa, wasije wakajitokeza baadaye na kulalamika kuwa wanaonewa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
No comments:
Post a Comment