Kwa sisi tuliosoma shule ya msingi zamani, Makari Hodari ni jina tunalolikumbuka sana. Tulisoma habari zake zilizotungwa na Padri Alfons Loogman, mwandishi wa vitabu vya Someni Bila Shida na Someni Kwa Furaha. Kwa kweli, padri huyu aliziteka nyoyo zetu watoto, akatufanya tupende kusoma. Aliandika vitabu kadhaa vya masomo ya ki-Swahili na hata mwongozo kwa walimu kuhusu kufundisha kusoma.Nakumbuka kuwa katika shule yangu ya msingi ya Litembo, tulikuwa tunasoma hadithi ya Makari Hodari kwa kuiimba. Watoto wote darasani tulikuwa tunaimba kwa pamoja, kwa furaha. Hadi leo naweza kuimba tulivyoimba. Na mwalimu alikuwa akiimba nasi. Pamoja na utamu wa hadithi, tulivutiwa na picha.
Nikiitafakari hadithi ya Makari Hodari, naona kuwa ilijengeka katika mfumo wa zile hadithi za kale za mashujaa, ambazo zinasimuliwa katika tamaduni mbali mbali. Kwa mfano, Wa-Haya wana hadithi za mashujaa kama Mugasha, Rukiza, na Kilenzi. Wa-Chagga wana hadithi ya Mrile, wa-Swahili hadithi ya Liongo Fumo. Hadithi ya Makari Hodari imerahisisha na kufupisha masimulizi ili yawavutie watoto kwa umri wao. Lakini inataja vitendo vya ushujaa, majigambo, na nafasi ya mama katika maisha ya shujaa.
Leo ni mara ya pili kwangu kuandika kuhusu vitabu hivi vya Padri Loogman katika blogu hii. Nilipoandika mara ya kwanza, ujumbe wangu uliwafikia watu wengi, hasa baada ya kutokea katika blogu ya Michuzi. Leo nimeona niwaletee wadau hadithi ya Makari Hodari, waione pia picha yake na picha ya mama yake.
8 comments:
Hahhaaaaaaaaaaa Katika siku ambazo umenikumbusha mbali basi ni leo hii.Asante sana
Duuhhh hahahahah umenikumbusha mbali sana,Ahsante sana, nipo na wanangu hapa naimba wao wanacheka tuu,nami nitajitahidi nivipate.
Mdau anonymous, shukrani kwa ujumbe wako. Tuko pamoja. Swahili na Waswahili, nimefurahi kuwa unawaburudisha wanao kwa wimbo wa Makari Hodari.
Kuwasomea watoto vitabu ni jambo ambalo nahamasisha sana. Nimeandika kuhusu jambo hilo katika blogu hii na pia katika kitabu changu kiitwacho CHANGAMOTO: Insha za Jamii, ambacho kinapatikana Dar es Salaam, simu namba 0754 888 647 na 0717 413 073.
yaani um,enifikisha mbali sana. Shukurani.Vipi hadithi ya Kishwira binti ya Sultani?
Unbakumbuka hadithi ya Nicolai Paganini? Imagine my surprise when Ilater leaned that Nicolo Paganini was an actual Italian Composer> My God I will forever tyreasure my Primary education.
Kofia yenye Mreri>
Wadau naona mmenifany nijikune kichwa, kwa kumbukumbu zenu za kusisimua. Kishwira binti Sultani yaonekana nimesahau. Paganini nakumbuka kiasi. Kofia yenye Mreri ndio sikumbuki kabisa. Lakini ni changamoto, maana natamani sasa kuanza kutafuta habari hizo.
Enzi zetu, shule ilikuwa shule kweli. Walimu walikuwa makini, na walipenda tufanikiwe, hata kwa bakora. Vinginevyo, bila hizo bakora, siamini kama ningefika hapa nilipo.
umenikumbusha hadithi za kwetu buhaya na sio hadithi ni vitu vilivyotokea kweli enzi na enzi ila wazee wetu zamani walikuwa hawaandiki lakini walikuwa wakariri sio kawaida sasa katika hizo hadithi kuna,kagoro,wamara hawa walikuwa wanadamu wenye karama nyingi na mpakasasahivi tunawafanyia matambiko
Post a Comment