Tuesday, March 13, 2012

Nimetua Bongo, Na "Laptop" Yangu Imetoweka

Nimetua Bongo kutokea ughaibuni tarehe 3 Machi. Wiki moja baadaye, "laptop" yangu imeibiwa hapa Dar es Salaam, eneo la Sinza. Ilikuwa ni Apple mpya. Nilikuwa nimeipakia maandishi yangu mengi, miswada na ripoti za utafiti wa kuanzia 1993.

Ninachohitaji ni haya maandishi. Huu ni mchango wa taaluma ambao natoa kwa wa-Tanzania na walimwengu. Miswada ya vitabu viwili nilitaka kuchapisha hapa Tanzania wakati huu, kwa manufaa ya wanafunzi, walimu, na jamii.

Hii "laptop" ukiifungua inakupa jina la Joseph Mbele, na unahitaji "password" ili kuweza kuitumia.

Habari ndio hiyo. Hivi sasa najiona kama mkulima mwenye ari ya kulima, lakini jembe hana. Nakala za miswada ziko ofisini Marekani. Lakini mimi nilipania kufanya kazi kubwa kwa wiki hizi nitakapokuwa hapa Tanzania. Nimekwama.

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

pole sana na natumaini aliyeiba atakurudishia..

tz biashara said...

Profesa Mbele pole sana hayo ndio maisha ya duniani hakuna tena sehemu inayoaminika,dunia yote imechafuka hata ulaya vilevile kuna wizi sana siku hizi.Kuwa muangalifu sana maana huko kwetu ndio hatari zaidi unaogopa hata kupokea simu ukiwa nje huna raha mtu au kwa maana nyingine naweza kusema hakuna uhuru kwa kuogopa wizi.

Naomba kukuuliza profesa maana siku hizi naona kuna mapaswad mawili hata kwa michuzi ni kwanini eti?Yaani yanaudhi sana huwa yanakufanya uwe mvivu wa kuchangia wakati mwingine kwasababu hukataa mara kwa mara inabidi urudie hata mara tatu au nne hivi.

Simon Kitururu said...

Pole sana!

Anonymous said...

Pole sana Profesa. Hakuna mtu anayeweza kukutumia nakala za miswada kwa email/dropbox?

Chemi Che-Mponda said...

Pole sana!

Anonymous said...

pole sana profesa ndio dsm hiyo lakini unaambiwa tumeweza tumesonga mbele

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...