Kuenesha blogu sio kazi rahisi. Kuna changamoto nyingi. Kwa mfano, wakati mwingine unashindwa kujua uandike nini. Huna  wazo  kichwani. Wakati mwingine unaandika ukijiuliza  kama kweli uchapishe hicho unachoandika. Unajua fika kuwa chochote unachochapisha, kinasambaa  duniani  dakika hiyo hiyo.
Kuna pia upande wa  wasomaji,  yaani hao tunaowaita wadau wa blogu. Binafsi,  nawakaribisha wadau wanaotembelea blogu yangu. Unapoandika  makala  kwenye  blogu  yako,  huwezi  kujua  watu  wataipokea vipi. Kila  mtu ni tofauti  na  mwingine.  Kinachomridhisha au  kumpendeza huyu  kinaweza  kumuudhi  mwingine. Ufanyeje  hapo?
Huwezi kumridhisha kila mtu, na kwa upande wangu siandiki kwa lengo la kumridhisha  yeyote. Najaribu tu kuelezea kilichomo akilini au moyoni mwangu wakati ninapondika. 
Kuna pia wadau wanaoandika maoni. Hapo pana changamoto. Kuna watoa maoni ambao wanamshambulia au kumbeza mwendesha blogu. Je, ni sahihi kwa mwendesha blogu kuyafuta maneno yao yasionekane kwenye blogu? Binafsi, naona ni bora watu wawe na fursa kamili ya kujieleza. Tatizo tu ni jinsi wengi wao wanavyojificha chini ya  kivuli cha anonymous. Mimi mwenye blogu najitambulisha wazi, na hata ninapoancika maoni kwenye blogu za wengine ninajitambulisha wazi, hata pale ninapoandika jambo linalowaudhi watu. Sielewi kwa nini wengine wasifanye hivyo hivyo. 
Lakini je, mdau akiandika  matusi dhidi ya mtu mwingine,  au akimdhalilisha mtu mwingine, ni sahihi  kuruhusu hayo kwenye  blogu yako? Suali  hili lilijitokeza  katika kikao changu na Mwenyekiti Mjengwa siku chache zilizopita.  
Nilijifunza mawili  matatu  kutoka kwake.  Ninajua  kuwa endapo  blogu  yangu itaendelea  na  kuwa  maarufu kama ya Mjengwa,  changamoto  za aina hii  zitanipata.
Nakaribisha uzoefu na maoni ya wanablogu wengine, na  ya  wadau.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
 
- 
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
- 
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
- 
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
 
 
 
5 comments:
Mimi (anonymous) nadhani kila blog ina watu wake wenye hadhi fulani.Kwa mfano hii blog yako Prof si rahisi kukuta ni sehemu ya wahuni wasio kuwa na nidhamu au wale watu wenye kujihisi ni lazima atoe maoni kwa kila kinachoandikwa.Unaweza ukaandika makala humu na watu wachache wakatoa maoni yao kistaarabu hata kama mtu atatofautiana na ww. Lakini makala hiyo hiyo ikatolewa kwenye blog nyegine utakuta jinsi watu wanavyo respond differentely.Hapo basi ndipo utakapo ona tofauti ya blog na watu wake.Si kila anonymous ataandika kumtukana mtu na si kila anyeandika jina lake huandika kiustaarabu bila ya kumtukana mtu. Hayo ni maoni yangu"anonymous"
Asante, anonymous, kwa mchango wako murua. Nimeguswa na kila ulilosema.
Profesa unacho kisema ndicho kilicho kwa baadhi ya watu,na ukweli usiyofichika kwamba ninapoandika nambo fulani ili wadau wa blog yangu wasome,ni kila mmoja atapokea aonavyo yeye,wengine watapendezwa nayo na wengine hawatapendezwa nayo.Lakini ahtuwezi kutumia mtandao huu ati kwa kuwa wengine wanachukizwa,ili mradi maadili ya matumizi ya mitandao inafuatwa.
Kuhusu kutumia lugha chafu kwenye mitandao ni ukosefu wa maadili,kwanini blog zitumike kuchafua wengine? Haipendezi.
Juma pili ya matawi njema.
Prof. Ulichosema ni kweli kabisa na kama alivyosema asiye na jina hapo juu kwamba inategemea na mtu na mtu sio hao wasio na majina tu ndio wanaoandioka lugha chafu ...na ni kwalöi utakuta mimi nineandika mada haileti changamoto lakini mada hiyohiyo mwingine anaichukua na kuiweka kibarazani kwake na inapokelewa na watu vingine kabisa....
Prof. Unachosema ni kweli. Binadamu tumezaliwa, na kulelewa katika mazingila tofauti. Aidha tunatofautiana ki elimu,imani, exposure na MTAZAMO. Ndio maana mtu mmoja anaweza kuiona glasi ya maji ikiwa NUSU imejaa na mwingine akaiona glasi hiyo ikiwa NUSU tupu. Glasi ni ileile kinachogomba ni mtazamo tu. Ni vizuri kuwaelewa watu na kuwachukulia jinsi walivyo.Ni vizuri kuonya, kukemea na kushauri kwa lugha nzuri. Hata hivyo tabia ya kutoa maoni ya matusi na kashfa dhidi ya watu wengine ni ukosefu wa ustaarabu na uduni wa kufikiri. Ni muhimu kumtendea mwingine unavyopenda kutendewa nawe.MWANADIKALA
Post a Comment