Monday, April 2, 2012

Nimetembelea Baruti, Dar es Salaam

Jana nilitembelea eneo la Baruti, Dar es Salaam. Hapa kushoto nimeweka picha ya msikiti niliouna pale, karibu na kituo cha dala dala, nami hupenda kupiga picha za nyumba za ibada. Ni sehemu muhimu kwetu waumini wa dini.







Nilienda Baruti kufuatilia ulizo la mwanablogu Rachel, alyeandika kwenye blogu hii, akitaka kujua kama Bahama Mama bado iko, nami nikampa ahadi kuwa ningeenda kuangalia. Nilikuta pamefungwa. Kwa nje hali ilionyesha kuwa ukarabati unaendelea, kama nilivyokuwa nimedokezwa. Niliishia kupiga pich ya kibao kinachoonekana hapa kushoto.

3 comments:

Rachel Siwa said...

Ohhhh Ahsante sana sana ndugu yangu kwa kazi kubwa na ya upendo kwangu,Mungu akubariki sana kaka Mbele kwa Yote!!

Mbele said...

Shukrani. Tulienda na ndugu yangu mmoja anayefahamu maeneo mbali mbali ya Dar es Salaam, na nilimweleza habari yote, akafurahi kuwa tulikuwa tunafanya jambo la kukuburudisha roho. Nakutakia kila la heri.

Rachel Siwa said...

Ahsanteni sana wapendwa wangu kwa kuniburudisha roho,naomba umfikishie salam zangu.Pamoja ndugu yangu.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...