Tuesday, April 3, 2012

Duka Asili, Sinza

Hapa ni eneo la Sinza, Dar es Salaam, mbele ya hoteli ya Lion, ambayo ni hapo upande wa kulia. Pana duka liitwalo Asili. Linauza dawa za asili, kama vile Amana, dawa ya kutibum malaria; MamaPlus, dawa ya tumbo la uzazi; Asili-T, dawa ya kuongeza kinga dhidi ya magonjwa mwilini; BabaPlus, dawa ya nguvu za kiume. Vile vile duka hili linauza vyakula dawa kama vile rosella, mlonge (moringa), unga wa ubuyu na mafuta ya ubuyu.




Mmiliki wake, Humphrey Yona Kimaro, ni msomi, mpenda mazungumzo kuhusu mambo mbali` mbali ya maendeleo na jamii. Hapa dukani pake nimekutana na marafiki wake kadhaa, ambao nao ni makini katika mambo hayo. Humphrey anavyo baadhi ya vitabu vyangu. Kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences kimeshakuwa changamoto ya mijadala kwenye vikao jioni baada ya kazi. Kwa taarifa zaidi na mawasiliano, tembelea tovuti ya Asilia au piga simu 0767 445 410.

2 comments:

emu-three said...

Sasa hivi dawa za asili zinatangazwa, zinahifadhiwa kitaalamu,...lakini kuna wajanja wanauza majivu na masizi wakisngizia eti ni dawa, je TBS, au sijui nani wanaodhibiti dawa hizi, ni bora tukaingilia kati kabla ya watu kulishwa sumu

Mbele said...

Ninapendekeza wadau wapite hapa Duka Asili wajionee wenyewe na pia kuongea na mmiliki. Nilivyoona ni kuwa wateja wanaridhika na wanachokipata hapo, na wanaendelea kuja. Halafu, kati ya wasomi niliowaona kwenye vikao vya hapo mahali, yuko pia daktari. Hiyo kwangu ni dalili nzuri.

Ni kweli kuwa hapa nchini kuna matatizo ya aina unayoiongelea. Na hata maduka ya dawa za kimagharibi yanadiriki kuuza dawa zilizoisha muda wake, na hivi kuhatarisha maisha ya watu. TBS nimesikia ikilalamikiwa kwa kutokuwa makini na kadhalika.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...