Wednesday, April 25, 2012

Yenu Bar, Ubungo

Pale Ubungo, eneo la stendi ya dala dala, upande wa pili wa barabara ya Morogoro kuna baa kadhaa. Nilipokuwa nasoma Chuo Kikuu Dar, kuanzia mwaka 1973, tulikuwa tunatinga eneo hilo kukata kiu. Bia zilikuwepo, na chibuku pia, kama sikosei. Baa moja iliyojulikana sana ni Yenu Bar, ya mzee mmoja Mchagga, maafuru kama Mzee Manywele. Mwanzoni mwa mwezi wa nne, mwaka huu, nilipokuwa nateremka kutoka eneo la Kimara, niliona sherti nipige picha ya Yenu Bar. ili wengine walioifahamu zamani wapate kujikumbusha enzi zile. Enzi zile, wanafunzi wa Chuo Kikuu tulikuwa makini sana katika masomo. Kwa hivi, ni baada ya kazi nzito ndio tulikuwa tunavinjari maeneo kama Yenu Bar, sio vingine.

2 comments:

John Mwaipopo said...

hapo pana ugali rosti (roast) baab kubwa. tena hawana choyo endapo utaomba uongezewe pande la ugali. chap chap.

Anonymous said...

safi mzee Mbele maana hapo saakumi nambili asubuhi supu tiyari pamoja na mchemsho wa ndizi

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...