Sunday, April 29, 2012
Vazi la Taifa
Jioni moja, mwezi uliopita, nikiwa natembea kwenye mtaa moja eneo la Sinza, Dar es Salaam, nilikutana na m-Maasai. Aliniuliza iwapo nimekutana na wa-Maasai wawili kwenye njia hiyo niliyotokea. Nilimwambia kuwa sijakutana nao.
Tutafakari suali la huyu m-Maasai. Ni wazi alijua kuwa m-Maasai anafahamika popote alipo. Mavazi yake yanamtambulisha. Ndio maana aliniuliza alivyoniuliza.
Huwezi ukamwuliza mtu Dar es Salaam iwapo amekutana na wa-Nyakyusa wawili, au wa-Chagga wawili, au wa-Matengo wawili. Hawatambuliki kama anavyotambulika m-Maasai. Picha niliyoweka hapa, ambayo inawatambulisha hao watu wawili, niliipiga Morogoro, eneo la stendi kuu ya dala dala.
Nawajibika kusema kuwa kuhusu suala hili la vazi la Taifa, wa-Tanzania tumepotea njia, kama walivyopotea wengine wengi kuanzia enzi za ukoloni. Kuna jambo ambalo tunaweza kujifunza kutoka kwa wa-Maasai.
Katika kutafakari suala hili, turejee kwenye kauli ya Frantz Fanon, mwanafalsafa na mtaalam wa masuala ya jamii, hasa zile zilizoathirika na ukoloni, ambaye tulikuwa tunamsoma sana enzi za ujana wetu, lakini sijui kama wa-Tanzania wa leo wanamsoma. Anasema hivi:
The way people clothe themselves, together with the traditions of dress and finery that custom implies, constitutes the most distinctive form of a society's uniqueness, that is to say the one that is the most immediately perceptible....
It is by their apparel that types of society first become known, whether through written accounts and photographic records or motion pictures. Thus, there are civilizations without neckties, civilizations with loin-cloths, and others without hats. The fact of belonging to a given cultural group is usually revealed by clothing traditions....(Frantz Fanon, A Dying Colonialism, trans. Haakon Chevalier, New York: Grove Weidenfeld, 1965, uk.35).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
4 comments:
Hii nimeipenda sana tena sana wengi huwa hatufikirii hili ni kweli ni ngumu kujua kama mimi ni m-NGONI...nimejifunza mengi hapa darasani leo. usengwili sana!!!
Napenda sana kuperuzi kwenye blog hii mara kwa mara hasa pale ninapokuwa sina idea ya nini niandike kwenye uchambuzi wangu. Hongera sana Prof. Mbele...
Bishop J. Hiluka
Dada Yasinta, shukrani kwa ujumbe wako. Anonymous, nafurahi kusikia unapitapita hapa kijiweni pangu. Karibu sana, na jisikie huru kuchangia.
Bishop J. Hiluka,
Asante sana kwa ujumbe wako. Nafurahi kusikia unasoma blogu yangu hii. Samahani niligilibika, nikachelewa namna hii kujibu. Lakini, nikitafsiri usemi wa ki-Ingereza, bora kuchelewa kuliko kuacha kabisa.
Leo, nimekutafuta mtandaoni, nikaiona tovuti ya Hiluka Filmz. Nimeipenda. Imenisaidia kuzifahamu shughuli zako. Nakutakia kila la heri.
Post a Comment